Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mheshimiwa Giuseppe Sean Coppola, aliyemtembelea Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Balozi huyo aliambatana na ujumbe kutoka Danieli Group, kampuni inayoongoza duniani katika teknolojia na uhandisi wa uzalishaji wa chuma, ambao wameonesha nia ya kuchunguza uwezekano wa kuwekeza katika sekta ya chuma nchini Tanzania.
Katika mazungumzo hayo, ujumbe huo uliwasilisha nia ya kuanzisha mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kisasa na kikubwa cha chuma mkoani Mtwara, kwa kushirikiana na mwekezaji mzawa.
Ushirikiano huu unatokana na majadiliano ya awali yaliyofanyika wakati wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia, pamoja na mashauriano ya kitaalamu yaliyofuata na taasisi za Tanzania, ikiwemo Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji Tanzania (TISEZA) na wizara husika.
Mradi unaopendekezwa, ambao bado uko katika hatua ya awali ya uchambuzi,
unakadiriwa kugharimu takribani Euro bilioni 1.5 (sawa na takribani Shilingi trilioni 4.2 za Kitanzania), na unatarajiwa kutekelezwa kwa awamu kulingana na tathmini zaidi na taratibu za uwekezaji.
Akizungumza katika kikao hicho, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alikaribisha nia hiyo na kusisitiza dhamira ya Tanzania kuendeleza uwekezaji wa kimkakati unaoendana na vipaumbele vya taifa.
“Tanzania inaendelea kujijenga kama kituo shindani na cha kuaminika kwa uwekezaji,ikitegemea rasilimali zake asilia, nafasi yake ya kimkakati, pamoja na mageuzi yanayoendelea kuboresha mazingira ya biashara,” alisema.
1/2Aliongeza kuwa, “Tunakaribisha ushirikiano unaoongeza thamani ya rasilimali zetu,unaozalisha ajira kwa wananchi wetu, na kuchangia dira yetu ya muda mrefu ya kujenga uchumi wa viwanda.”
Kwa upande wake, Balozi wa Italia alieleza kuwa ushirikiano huo unaakisi kuimarika kwa mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Italia chini ya mifumo mipana ya ushirikiano wa maendeleo.
“Nia iliyooneshwa na Danieli Group ni sehemu ya juhudi pana za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, ikiwemo kupitia Mpango wa Mattei kwa Afrika,” alisema.
Aliongeza kuwa, “Mpango huu unalenga kukuza uwekezaji endelevu na wenye manufaa,kwa pande zote, na Tanzania inaonekana kuwa mshirika muhimu katika muktadha huu.
Kwa sasa, tupo katika hatua ya kuangalia uwezekano na tunatarajia kuendelea
kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Tanzania kadri majadiliano yatakavyoendelea.”
Naye Mtendaji Mkuu wa Danieli Group, Bw. Giacomo Mareschi Danieli, alieleza sababu za kimkakati zilizoifanya kampuni hiyo kuvutiwa na Tanzania.
“Tunaona fursa kubwa nchini Tanzania, si tu kutokana na uwepo wa rasilimali kama gesi na madini ya chuma, bali pia kutokana na ukuaji wa soko na nafasi yake ya kimkakati katika ukanda huu,” alisema.
“Mtazamo wetu unalenga ushirikiano wa muda mrefu - kuleta teknolojia ya kisasa
inayozingatia mazingira, huku tukishirikiana na wadau wa ndani kukuza ujuzi na
kujenga uwezo endelevu wa viwanda. Hii ni hatua ya awali, na tumejipanga kuendelea na majadiliano ya kitaalamu ili kutathmini uwezekano wa mradi huu,” aliongeza.
Iwapo utatekelezwa, uwekezaji huu unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ajenda ya Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda chini ya Dira ya Taifa ya 2050, kwa kuimarisha uzalishaji wa ndani wa chuma, kupunguza uagizaji kutoka nje, kuongeza thamani ya rasilimali za ndani, na kutengeneza ajira kwa vijana.
Aidha, unaweza kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha uzalishaji wa chuma
katika ukanda huu, hususan kwa nchi jirani zisizo na bandari, pamoja na kusaidia
maendeleo ya miundombinu na usafirishaji katika ukanda wa Mtwara.
Mheshimiwa Rais Samia alimhakikishia Mheshimiwa Balozi na ujumbe wake kuwa
Serikali itaendelea kuwa wazi kwa wawekezaji wenye sifa, wanaoleta si mtaji pekee bali pia teknolojia, ujuzi na dhamira ya muda mrefu katika maendeleo ya Tanzania.
Kikao hicho kimeonesha kuendelea kuimarika kwa mvuto wa Tanzania kama kituo cha uwekezaji, pamoja na dhamira ya pamoja ya pande zote mbili kuendele.

.jpeg)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mheshimiwa Giuseppe Sean Coppola, na ujumbe kutoka DANIELI Group, Ikulu, Dar es Salaam tarehe 29 Machi, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mkurugenzi na Mmiliki wa DANIELI Group Bw. Giacomo Mareschi-Danieli, Ikulu, Dar es Salaam tarehe 29 Machi, 2026..jpeg)

No comments:
Post a Comment