JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


UDOM, UNICEF WALETA MAPINDUZI YA KIDIJITALI KONDOA

Share This


Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Joseph, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Amani Abeid Karume kuhusu fursa za kujifunza kidijitali, wakati wakikagua huduma ya mtandao imavyofanya kazi shuleni hapo na kusaidia wanafunzi kujifunza.

....

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania, kimeanza kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya kidijitali katika Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, kupitia mradi wa kusambaza huduma ya intaneti kwa shule na jamii.

Katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo iliyofanyika leo Alhamisi, tarehe 19 Machi 2026, ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Mdami, imeelezwa kuwa hatua kubwa tayari imefikiwa.

Msimamizi wa mradi huo, Dkt. Jabhera Matogoro, amesema vituo 10 tayari vimeunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi ya 20Mbps, ikijumuisha shule tano za sekondari na Msingi, na vituo vitano vya jamii, hatua inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika upatikanaji wa taarifa, ujinzaji na ufundishaji.

Ameeleza kuwa mradi huo unalenga kuwezesha walimu, wanafunzi na wananchi kwa ujumla kupata maarifa kwa urahisi kupitia mtandao, sambamba na kuchochea fursa za ajira, ubunifu wa kibiashara na maendeleo ya kijamii katika wilaya hiyo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Joseph, akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa, Bi. Sekela Mwasubila, kuhusu utekelezaji wa mradi wa Huduma ya Mtandao inayotolewa kwa shule 5 na ofisi 5 za Kata.

Miundombinu ya teknolojia ya mawasiliano ya mawimbi ya microwave inayotolewa na kampuni ya Airtel, ikisambaza huduma ya intaneti yenye kasi ya Mbps 20, kupitia Mradi unaofadhiliwa na UNICEF.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Bukulu, Mwl. Joseph Paul, akieleza namna huduma ya mrandao inavyorahisisha ujifunzaji katika maabara ya kompyuta shuleni hapo.

Mkuu wa Shule ya Msingi Isabe, Mwl. Jackline Richard, akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa kusambaza huduma ya mtandao kwa shule na jamii.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Joseph, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Amani Abeid Karume kuhusu fursa za kujifunza kidijitali, wakati wakikagua huduma ya mtandao imavyofanya kazi shuleni hapo na kusaidia wanafunzi kujifunza.

Msimamizi Mkuu wa Mradi, Dkt. Jabhera Matogoro, akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Mdami, wakikagua matumizi ya huduma mtandao darasani kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Amani Abeid Karume iliyopo WIlayani Kondoa.

Msimamizi Mkuu wa Mradi, Dkt. Jabhera Matogoro, akitoa maelezo kuhusu utendaji wa teknolojia ya intaneti katika moja ya vituo vilivyonufaika na mradi huo, Chama cha Ushirika cha Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad