Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo tarehe 26 Machi 2026 amewasili Jijini Malabo nchini Guinea ya Ikweta, ambapo anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki, utakaofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Machi 2026.
Katika Mkutano huo, Tanzania itapata fursa ya kuwasilisha vipaumbele vyake vya Kitaifa pamoja na kuchangia kuunda mwelekeo wa mikakati mipya ya jumuiya hiyo, inayoelekea kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano huo ni mwendelezo wa jitihada za kuendelea kushiriki kikamilifu katika majukwaa ya kikanda na kimataifa, na kudhihirisha mchango wa nchi katika mijadala ya maendeleo na ushirikiano wa kimataifa.
Aidha, Makamu wa Rais anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano huo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kimaendeleo.
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)





.jpeg)



No comments:
Post a Comment