JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


HALOPESA YAGUSA FAMILIA ZAIDI YA 60 KUELEKEA SIKUKUU YA EID (KIBAHA, PWANI)

Share This

Katika kuadhimisha Sikukuu ya Eid El Fitr, HaloPesa imeendesha zoezi maalum la kijamii (CSR) kwa kutoa msaada wa mahitaji muhimu kwa familia zaidi ya 60 katika Kata ya Visiga (Visiga A na Visiga B), Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Mpango huu ulilenga kusaidia familia zenye uhitaji kwa kuwapatia mahitaji ya msingi ya chakula ikiwemo mchele, mafuta ya kupikia, sukari pamoja na bidhaa nyingine muhimu, ili kuwawezesha kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa furaha, amani na heshima.

Tukio hili liliongozwa na Meneja Masoko wa HaloPesa, Bi. Aidat Lwiza, kwa kushirikiana na Meneja wa Halotel Mkoa wa Pwani, Bw. Rodrique Paul, pamoja na timu ya Halotel. Aidha, tukio lilihudhuriwa na viongozi wa serikali za mitaa akiwemo Diwani wa eneo hilo, Mhe. Mohamed Mpaki, pamoja na wenyeviti wa maeneo husika, Bw. Ibrahim Saidi na Bw. Elisha John, waliojitokeza kuunga mkono jitihada hizi za kusaidia jamii.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Bi. Aidat Lwiza alisema:

"Mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kipindi cha kuonesha upendo, huruma na mshikamano.

HaloPesa inaamini kuwa mafanikio ya biashara yanaenda sambamba na ustawi wa jamii.

Kupitia mpango huu, tunalenga kugusa maisha ya familia hizi na kuhakikisha wanasherehekea Eid kwa furaha na amani zaidi."

Kwa upande wake, Bw. Rodrick Paul alieleza:

"Ushirikiano huu unaonesha dhamira ya dhati ya kampuni ya Halotel kwa ujumla katika kuendelea kuwa karibu na jamii, kujenga mshikamano na kusaidia wale wenye uhitaji katika maeneo tunayohudumia."

Diwani wa kata hiyo, Mhe. Mohamed Mpaki, aliipongeza HaloPesa kwa jitihada hizo na kusisitiza umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na jamii katika kuleta maendeleo jumuishi.

Kupitia mpango huu, Halotel, HaloPesa inaendelea kuthibitisha kuwa ni zaidi ya huduma za mawasiliano na kifedha bali ni mshirika wa karibu anayejali na kugusa maisha ya watu na jamii kwa ujumla.

HaloPesa – Tunajali, Tunathamini.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad