
KAMPUNI ya kimataifa ya michezo ya kubashiri na burudani ya kidijitali, iliyokuwa ikijulikana kama Golden Matrix Group, inaelekea kubadilisha jina lake rasmi na kuwa Meridian Holdings Inc. Inatarajiwa kwamba kuanzia tarehe 3 Machi 2026, kampuni hiyo itaanza kufanya biashara katika soko la Nasdaq Capital Market chini ya alama mpya ya hisa MRDN. Hatua hii inaashiria mwanzo mpya wa kimkakati unaolenga kuimarisha taswira ya kampuni katika soko la kimataifa na kuvutia wawekezaji wakubwa zaidi.
Mabadiliko haya ni sehemu ya mkakati wa kuoanisha utambulisho wa kampuni na chapa yake kuu na yenye nguvu zaidi duniani, Meridianbet. Baada ya kipindi cha ukuaji wa kasi na kuimarika kwa shughuli zake, kampuni sasa inajumuisha taasisi sita muhimu ambazo ni Meridianbet, Expanse Studios, RKings, Classics for a Cause, GMAG na Mexplay. Muunganiko huu unaonyesha uimara katika sekta ya michezo ya kubashiri, burudani na teknolojia.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Mageuzi haya ya kibiashara yamekuja muda mfupi baada ya Meridianbet kufanikisha ununuzi wa asilimia 100 wa kampuni ya Fairbet Ltd., mwendeshaji aliyeidhinishwa wa michezo ya kubahatisha nchini Malta. Kupitia ununuzi huo, Meridianbet imeongeza mara mbili uwepo wake katika maeneo ya Malta na Gozo ikiimarisha nafasi yake kama mwajiri na mtoa huduma mkubwa katika soko hilo.
Sambamba na hatua hiyo, Meridian Holdings Inc. pia inategememea kutangaza mpango wa kuunganisha hisa ili kuboresha muundo wake. Mkakati huu unalenga kuongeza mvuto wa hisa zake kwa wawekezaji wa taasisi na kuoanisha thamani ya hisa na viwango vya kimataifa vya sekta ya michezo ya kubahatisha. Hii ni ishara ya dhamira ya kampuni katika kujenga msingi imara wa kifedha kwa ajili ya upanuzi endelevu wa muda mrefu.
Akizungumzia mabadiliko hayo, Afisa Mtendaji Mkuu, Zoran Milosevic, amesema kuwa mabadiliko ya kuwa Meridian Holdings yanaakisi hali halisi ya biashara ya kampuni leo. Amesisitiza kuwa kwa Meridianbet kuwa chapa kinara na kwa kuzingatia mafanikio ya upanuzi nchini Malta, kampuni imeamua kuunganisha utambulisho wake ili kuwahudumia vyema zaidi wanahisa wake na masoko yote inayofanyia kazi.


No comments:
Post a Comment