JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Atletico Madrid Kumaliza Nafasi ya Ngapi Msimu Huu?

Share This

 


LIGI kuu ya Hispania yaani LALIGA inazidi kupamba moto huku wakali wa ubashiri leo watakupatia uchambuzi wa Atletico Madrid ambao wameuwa na fomu nzuri msimu huu na uwezekano wa kuondoka na taji lolote msimu huu.

Timu huu ambayo ipo chini ya kocha mkuu Diego Simeone wamaeendelea kuwa moja ya timu zenye heshima kubwa barani Ulaya, lakini msimu wao wa sasa unaonyesha wazi kuwa wako kwenye kipindi cha mpito kati ya ubora wa zamani na ushindani wa kisasa.

Atletico Madrid imejijengea utambulisho wa uimara wa kujilinda na nidhamu ya hali ya juu, lakini changamoto zinazoikabili sasa zinaonyesha wazi kuwa mfumo huo unahitaji maboresho ili kuendana na kasi ya mpira wa leo.

Kwenye LaLiga, Atletico Madrid wamekuwa wakipambana kubaki kwenye nafasi za juu ambapo hadi sasa wapo nafasi ya 4 baada ya kukusanya pointi zao 57 kwenye michezo 29 ambayo wamecheza na wakiwa nyuma kwa pointi 16 kwa kinara wa ligi.

Wapo nyuma ya vigogo kama Real Madrid na Barcelona, jambo linaloonyesha pengo lililopo katika consistency. Mara nyingi wanapoteza pointi muhimu dhidi ya timu ndogo hili ndilo tatizo kubwa linalowafanya washindwe kusimama kama wagombea halisi wa taji. Ugenini wamekuwa wakionyesha udhaifu mkubwa, tofauti na uimara wao wanapocheza nyumbani.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Timu hiyo ina wachezaji wazuri sana ambao hufanya vyema kwenye mechi kubwa na safari hii imeongeza wachezaji kama Ademola Lookman ambaye ataenda kusaidiana na kina Solorth, Giuliano Simeone, Koke na wengine kibao.

Julian Alvarez ambaye pia alijiunga na timu hiyo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho, lakini pia ni mchezaji ambaye anahitaji sana na baadhi ya timu kutoka Uingereza ikiwemo, Chelsea, Arsenal na zingine. Lakini mpaka sasa bado mustakabali wake hujajulikana.

Kwa upande wa Antoine Griezman naye pia amekuwa na mchango mkubwa kalbuni hapo lakini anaondoka mwishoni mwa msimu huu na tayari amesaini mkataba wa kuitumikia Orlando City ya Marekani hivyo Madrid watajitaji kusaka mchezaji mwingine kuziba pengo hilo.

Simeone na vijana wake kwenye mashindano ya Copa del Rey wamefanikiwa kufika hatua ya Fainali baada ya kumtoa Barcelona na watakipiga dhidi ya Real Sociedad April 18, hili ni Kombe ambalo wanalitaka kwa hali na mali kutokana na ushindano uliopo kwenye mashindano mengine. Je Atletico watabeba Kombe hili?. ODDS KUBWA izpo Meridianbet ingia na ubeti sasa.

Atletico Madrid kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya yaani UEFA Champions League, wameendelea kufanya vizuri ambapo mpaka sasa wapo hatua ya Robo Fainali na wamepangwa kucheza dhidi ya FC Barcelona hivyo badi Simeone ana kibarua kizito kabisa mbele ya vijana wa Hans Flick.

Ni mechi ngumu kabisa lakini pia kama wakichanga karata zao vizuri wanaweza wakaibuka na ushindi kwani hii si mara ya kwanza kukutana hawa wawili. Je unadhani Barca watakubali kutolewa kwenye UEFA?. Bashiri hapa.

Kwa ujumla, Atletico Madrid ni timu ambayo bado ina uwezo wa kushindana katika mashindano yote, lakini imekosa ule uthabiti wa kuwa mabingwa. Ili kurejea kileleni, wanahitaji kuongeza ubunifu katika safu ya ushambuliaji, kupunguza utegemezi kwa mchezaji mmoja, na kubadilika kimfumo ili kuendana na mahitaji ya soka la kisasa. Bila kufanya hivyo, wataendelea kubaki kwenye kundi la timu bora lakini si mabingwa wanaotawala.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad