JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Serengeti Apple Yaongoza Shamrashamra za Siku ya Valentine Jijini Dar es Salaam

Share This

Serengeti Breweries Limited (SBL) imeendelea kuimarisha mkakati wake wa ubunifu wa kupitia Serengeti Premium Apple — kinywaji chake kipya kilichotengenezwa hapa Tanzania — kwa kuongoza shamrashamra za Siku ya Valentine kupitia matukio maalum jijini Dar es Salaam.

Ikiwa imelenga kuwashirikisha zaidi wateja na watumiaji zake kupitia matukio tofauti, chapa hiyo iliendesha mfululizo wa hafla katika maeneo mbalimbali ya jiji. Galentine’s iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana ilikuwa tukio kuu lililowaleta pamoja wateja, washirika na wageni waalikwa kusherehekea urafiki, mafanikio na kinywaji kipya chenye hadhi ya juu inayoendana na maisha ya kisasa. Tukio hilo liliimarisha nafasi ya Serengeti Premium Apple kama ubunifu wa Kitanzania unaokidhi mahitaji yanayobadilika ya walaji.

Mkakati huo uliendelea kupitia matukio kama vile Galentine’s Brunch iliyofanyika katika mgahawa wa Upper Deck pamoja na ushirikiano maalum wa Bravo Coco na Serena Hotel — yote yakiongozwa na Serengeti Premium Apple kama chapa kinara. Flaviana Matata, Balozi wa kinywaji hiki kipya, alikuwepo Johari Rotana kama sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya chapa na wateja, huku wageni waalikwa wakifurahia kinywaji lilikuwa ni tukio ambalo lilibeba dhana nzima ya hafla hiyo.

Jumapili, tukio la Big Brunch katika hoteli ya Ramada Resort iliongozwa na kinywaji cha Serengeti Lemon, ikionyesha upana wa bidhaa za SBL, wakati Smirnoff Ice iliwafikia wale ambao bado wako ‘single’ kupitia tukio la “Valentine’s Is a Vibe – Singles Rave.” Chapa nyingine zikiwemo Smirnoff Ice Vodka, Singleton Whisky na Gordon’s Gin nazo hazikuwa nyuma kwani ziliongeza nguvu katika kuwapatia wateja burudani na vibe la kipekee katika matukio ya wikiendi hiyo.

Kupitia mkakati huu wa shughuli za kipekee katika maeneo mbalimbali na ushirikiano wa bidhaa zake, SBL imeendelea kuonesha uwezo wake wa kutumia ubunifu, kuwashirikisha wateja na nguvu ya bidhaa zake nyingi kwa pamoja — huku Serengeti Premium Apple ikiimarika kama kichocheo muhimu cha ukuaji katika soko la vinywaji vyenye hadhi ya juu vinavyozalishwa hapa nchini Tanzania. #serengetiapple.
















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad