Na Nasra Ismail, Geita
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita leo Februari 3,2026 katika Mkutano wake wa Kawaida wa robo ya pili kwa mwaka 2025/26 limewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa ngazi ya kata.
Awali akizungumza katika baraza Hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri uliopo Nzera, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Karia Rajab Magaro amewapongeza madiwani hao kwa kupewa ridhaa na wananchi ili kuendelea kuisimamia Serikali katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa mujibu wa Kanuni,sheria na taratibu zilizowekwa.
"Tufanye kazi kwa kushirikiana ili kuweza kufanikisha shughuli za Halmashauri" Amesema Bw. Magaro.
Vilevile Magaro ametoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na watendaji katika Kata zao kufanya vikao na kuwa na taarifa za mapato na matumizi kwa ustawi wa Halmashauri.
"Taarifa za mapato na matumizi ni muhimu sana hivyo nitoe wito kwenu kuzisimamia kwa kushirikiana na watendaji" Amesema Bw Magaro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Nkome Mhe Christopher Kahesi amewataka Madiwani kuwa mfano mzuri kwa kuzingatia na kuzifuata kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ili kuwa na viwango vizuri.
Pamoja na hayo Mhe Kahesi katika Mkutano huo amewasihi Madiwani kuendelea kutoa ushirikiano katika kata nyingine ambazo zina changamoto ili kuzitatua kwa ushirikiano kwa maslahi ya Halmashauri.
.jpeg)

.jpeg)



.jpeg)

.jpeg)



.jpeg)



No comments:
Post a Comment