JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KITETO WAAHIDIWA KUPATIWA MWENYEKITI WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA LA WILAYA

Share This

Na Munir Shemweta, KITETO


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo ameahidi kupelewa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.

Dkt Akwilapo alitoa ahadi hiyo leo tarehe 26 Februari 2026 kufuatia kuwasilishwa kwa malalamiko na mwananchi mmoja aliyemueleza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba aliyeko katika ziara mkoani Manyara kuwa, katika wilaya ya kiteto wananchi wamekuwa wakipata shida ya kushughulikiwa mashauri yao ya ardhi kupitia Baraza la Ardhi kutokana na kukosekana kwa mwenyekiti wa Baraza.

Kwa sasa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kiteto linahudumiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba kutoka Dodoma jambo lililoelezwa kuwa limechangia mashauri kuchukua muda mrefu.

Dkt Akwilapo amesema, suala la Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya katika wilaya ya Kiteto tayari limeshamfikia na analifanyia kazi na muda wowote mwenyeikiti atapatikana ndani ya muda mfupi.

‘’Nimemuagiza katibu mkuu aliyefanyie kazi na muda wowote tutapata mwenyekiti mahsusi kwa ajili ya eneo hili’’. Amesema Dkt Akwilapo

Akigeukia suala la migogoro ya ardhi katika wilaya ya Kiteto, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema, migogoro mingi katika wilaya ya Kiteto imesababishwa na ukosefu wa mipango ya matumizi ya ardhi.

Kwa mujibu wa Dkt Akwilapo, wilaya ya Kiteto ina jumla ya vijiji 63 na kati ya hivyo vijiji 33 ndivyo vilivyofanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi huku vijiji 22 mpango wake ukiwa umeisha muda wake jambo alilolieleza kuwa, sasa jumla ya vijiji 52 vinahitaji kufanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi.

Amesema, Wizara yake inalifanyia kazi suala hilo na katika mpango wa Bajeti ijayo ya 2026/2026 wameomba fedha na itakapofanikiwa Wizara yake itatekeleza mpango huo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba wilayani Kiteto mkoani Manyara tarehe 26 Februari 2026.
Waziri Mkuu Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akiwa pamoja na viongozi wengine wakati wa ziara yake mkoani Manyara tarehe 26 Februari 2026. Wa pili kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara katika ziara ya Waziri Mkuu Wilayani Kiteto mkoani Manyara tarehe 26 Februari 2026.
Waziri Mkuu Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akisalimiana na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri alipowasili wilayani Kiteto wakati wa ziara yake mkoani Manyara tarehe 26 Februari 2026. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad