Mkurugenzi Mkuu wa Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Profesa Najat Kassim Mohammed akizungumza kuhusiana na ujio wa IAEA katika Taasisi ya Ocean Road kuangalia mashine za miozi, jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ocean Road Dkt.Diwani Msemo akizungumza kuhusiana na mikakati ya Taasisi mara baada ya kutembelewa na IAEA jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kiufundi kwa Afrika Gashaw Gebeyehu Wolde wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA)akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembembelea mashine za kisasa katika Taasisi ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
*Waahidi kuwa wa kwanza kudhibitisha Ithibati ya ubora.
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) limesema kuwa Taasisi ya Ocean Road imefanya mageuzi katika utoaji huduma za saratani.
Akizungumza katika ziara ya Shirika hilo likiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kiufundi kwa Afrika Gashaw Gebeyehu Wolde amesema Taasisi ya Ocean Road katika imefanya mageuzi makubwa ya kuwa na vifaa vya teknolojia katika otoaji wa huduma za Saratani ikilinganishwa na miaka iliyopita wakati walipotembelea.
Wolde amesema katika hatua ambayo imefikiwa watakuwa watu kwanza katika kupitisha ithibati ya ubora ya huduma ya Saratani na kufanya Taasisi ya Ocean Road kuwa ya Tatu Afrika katika utoaji huduma hiyo.
Amesema Serikali ya Tanzania imewekeza katika kuwa na miundombinu pamoja na vifaa vya Kisasa ikiwemo za ugunduzi wa saratani za aina mbalimbali.
Aidha amesema IAEA itaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) ili kuimarisha ushirikiano, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya matumizi ya mashine za CT-Scan na kutoa vifaa vya mionzi na kusomesha wataalam katika ubobezi wa magonjwa ya saratani.
Hata hivyo Wolde ametoa shukurani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ununuaji wa mashine za kisasa na fedha nyingi katika Taasisi ya Ocean Road.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ocean Road Dkt.Diwani Msemo amesema kuwa ujumbe IAEA wametembelea mashine mbalimbali na kuona Taasisi hiyo imejipanga.
Amesema miundombinu na vifaa tiba vilivyopo vimeongeza huduma katika kutoa huduma kwa mgonjwa bila kuathiri .
Hata hivyo amesema ujumbe huo umekiri kuwa mashine zilizopo za kisasa katika hospitali za Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu wa Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Profesa Najat Kassim Mohammed amesema Taasisi ya Ocean Road imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma ya Saratani.


.jpeg)
.jpeg)



No comments:
Post a Comment