JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


GF YAADHIMISHA MIAKA 19 YA KUANZISHWA KWAKE,ASILIMIA 90 YA WAFANYAKAZI NI WAZAWA.

Share This

Katika kuadhimisha miaka 19 ya kuanzishwa kwa kiwanda cha kuunganisha magari cha GF, uongozi wa kiwanda hicho umesema unajivunia kuwa sehemu ya kuzalisha ajira, huku ukieleza kuwa asilimia 90 ya wafanyakazi wake ni wazawa.


Akizungumza na waandishi wa habari, leo Februari 07, 2026, makao makuu ya kiwanda hicho yaliyopo Kibaha mkoani Pwani, Meneja Mkuu wa kiwanda cha GF, Ezra Mereng, amesema miaka 19 ya dira na matumaini yalianza kama ndoto, lakini hadi sasa kiwanda hicho kinajivunia kuzalisha magari ya aina mbalimbali.

“Leo tunajivunia kusherehekea miaka 19 ya GF, na sisi kama kiwanda tunajivunia kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wafanyakazi ni vijana wazawa wa hapa Tanzania waliotoka katika vyuo mbalimbali hapa nchini."

Naye Meneja Chapa na Masoko wa GF Group, Salman Karmal  pamoja na kufurahia mafanikio ya kiwanda hicho, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za uwekezaji zinazowavutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini.

Amesema katika kuadhimisha miaka 19 ya GF, kiwanda hicho kimekuja na mpango wa kurudisha kwa jamii, ambapo wameanza kwa kutembelea watu wenye mahitaji maalumu pamoja na kufadhili timu ya mpira wa miguu ya Nyumbu FC iliyopo jirani na kiwanda hicho, ambayo imekuwa ikifanya vizuri kwenye michezo yake mbalimbali.

“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuweza kufungua milango rafiki ya uwekezaji inayotufanya tuwe na uthubutu wa kujiimarisha zaidi katika maeneo mbalimbali ya kibiashara".

Kwa upande wake, Sefroza Mwizarubi, ambae ni mnufaika wa program ya kuchukua wanafunzi vyuoni , amewashukuru viongozi wa GF kwa kutoa nafasi kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali kwenda kujifunza namna ya kuunganisha magari, jambo linalowafanya kuwa wabobezi katika nyanja hiyo.

“Mimi ni mnufaika wa mpango wa GF wa kuchukua wanafunzi kutoka vyuoni kwa ajili ya kuja kupata ujuzi wa kuunganisha magari, lakini pia kupata ajira,” amesema Mwizarubi.
Meneja Mkuu wa kiwanda cha GF Vehicle Assemblers,  Ezra Mereng akizuingumza na wafanyakkazi wa kiwanda hicho wakati wa hafla ya madhimisho ya miaka 19 ya kampuni ya GF mkoani Pwani




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad