JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Elimu ya Mirathi Yatajwa Kama Kinga Dhidi ya Migogoro ya Familia

Share This
NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Mirathi Tanzania limepongezwa kwa kuanzisha programu ya utoaji elimu ya mirathi mashuleni ambayo inaenda kujenga msingi wa uelewa wa sheria kwa vijana wakiwa bado wadogo na kwenda kuwaelimisha na wengine.

Pongezi hizo zimetolewa leo Februari 3, 2026 Kigamboni Jijini Dar es Salaam na Ofisa Tarafa Wilaya ya Kigamboni Agusta Safari wakati akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo kwenye uzinduzi wa programu ya utoaji elimu ya mirathi mashuleni

“Hili ni wazo la kimapinduzi kwa sababu mnaanza kujenga msingi wa uelewa wa kisheria kwa vijana wetu wakiwa bado wadogo.Nawaasa wanafunzi wote wasikilize kwa makini elimu hii na kusomaJarida maalumu ambalo litagawanywa bure kwa wanafunzi.

“Elimu hii ambayo inatolewa na MITA wanafunzi hakikisheni mnaifikisha kwa wazazi wenu nawalezi wenu kikamilifu. Aidha namshukuru Balozi wa Ireland hapa Tanzania Ms. Nicola Brennan kwa ufadhili wa elimu hii.”

Kuhusu mantiki ya elimu ya mirathi kwa wa kwa Wanafunzi amesema imekuwa ikishuhudiwa mara nyingi familia zikisambaratika mara baada ya mzazi au mlezi kufariki dunia. Migogoro ya mirathi imekuwa chanzo kikubwa cha wanafunzi kuacha shule kwa kukosaada na mahitaji, watoto kufukuzwa kwenye nyumba walizozaliwakutokana na dhuluma.

Hivyo amesema hatua ya kuleta elimu hiyo mashuleni kwa sababu kwa upande mmoja wanafunzi ndio wahanga wakuu na pia ndio mabalozi bora wa mabadiliko kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.

Pamoja na hayo amesema Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejikita katika kusimamia haki za wanyonge, hususan wanawakena watoto. “Kampeni hii ni sehemu ya jitihada hizo za kuhakikisha hakuna mtoto anayekatishiwa ndoto zake kwa sababu ya dhuluma ya mali.”

Kwa upande wake Katibu Mkuu Mtendaji wa MITA amesema Rose Fusi amesema programu hiyo ya utoaji elimu ya mirathi mashuleni inalenga kuwapa vijana uelewa wa kisheria na kimaadili kuhusu usimamizi wa mali za marehemu na haki za warithi mapema kabla hawajakumbana na changamoto hizo katika maisha ya utu uzima.

“Taasisi ya MIRATHI TANZANIA (MITA) tunamshukuru Balozi wa Ireland hapa nchini, MS. Nicola Brennan, kwa kutoa ufadhili wa programu hii ya kutoa elimu ya mitathi mashuleni kwani ufadhili wake ni mbegu njema iliyopandwa kwenye ardhi ya Kigamboni ambayo itaota na kuzaa matunda mema kwa ustawi wa Taifa zima. “ Amesema

Akifafanua zaidi amesema programu hiyo pia inalenga kujenga uelewa huo ili kuweka kinga dhidi ya dhuluma na migogoro ya kifamilia kwa kuwa watoto watakuwa mabalozi wa haki na kuwa chachu ya mabadiliko chanya ya fikra kwa wazazi na walezi na kuchochea uandishi wa wosia.

Pia itachochea ulinzi wa amani ya familia na kuhakikisha wajane na watoto yatima hawadhulumiwi haki zao. “Zao la programu hii ni kujenga jamii inayoelewa sheria za mirathi na kupunguza mzigo wa kesi za madai na jinai mahakamani.

Fusi amesema elimu ya mirathi kwa wanafunzi itahakikisha rasilimali (kama ardhi, fedha na biashara) zinaendelea kutumika kwa tija hata baada ya mmiliki kufariki, hivyo kukuza pato la taifa.

Akifafanua zaidi amesema kuelekea Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, wanalenga kuwa na jamii yenye utawala wa sheria na usawa wa kijamii na kiuchumi. “Kwa kuwa Dira ya 2050 inategemea pakubwa katika uwekezaji, bila elimu ya mirathi,uwekezaji wa wazazi hupotea mikononi mwa warithi wasio na uelewa au kupitia dhuluma.

“Hivyo kuweka msingi wa uelewa wa mirathi kwa kila mwananchi kunachochea upatikanaji wa haki yake ya urithi ambayo ni sehemu ya mkakati wa kupunguza umaskini na kukuza mtaji kwa kizazi kimoja kwenda kingine.”

Wakati huo huo Cainess Samweli ambaye ni Ofisa Ustawi was Jamii Wilaya ya Kigamboni amesema kuwa elimu hiyo ambayo imezinduliwa mashuleni itakwenda kuamsha uelewa kwa jamii na hivyo kuepusha migogoro inayotokana na mirathi iliyoachwa katika familia.

Kwa upande wao wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nguva wamesema kutolewa kwa elimu ya mirathi mashuleni wanaamini wanafunzi wengi watakuwa na uelewa huku wakieleza kuna baadhi ya wanafunzi wamekatisha masomo kutokana na migororo ya mirathi ambayo imejitokeza katika familia zao.










No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad