JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


CMSA:SERIKALI IMEPATA MAFANIKIO MAKUBWA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA

Share This

 -Katika kipindi cha mwaka 2025 imefikisha Sh.trilioni 4.4 kutoka Sh.trilioni 2.6 

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) imesema Serikali imepata mafanikio makubwa kupitika mifuko ya uwekezaji ya pamoja ambapo katika kipindi cha mwaka 2025 imefikisha Sh. trilioni 4.4 ikilinganishwa na Sh.trilioni 2.6 ya mwaka 2024.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Usimamizi na Uchunguzi wa Mamlaka hiyo Exaud Julius katika hafla wadau wa sekta hiyo kutathimini utendaji wa masoko ya mitaji kwa mwaka uliopita.

“Hatua hiyo imetokana na Serikali kuweka mazingira wezeshi na shirikishi yenye lengo la kukuza na kuendeleza masoko ya mitaji pamoja na matumizi ya tehema.CMSA imepata mafanikio makubwa mwaka 2025, kutokana na ushirikishwaji mzuri wa wadau na sera zinazounga mkono na kuboresha mazingira ya uwekezaji.”

Ameongeza pia matumizi ya teknolojia na ubunifu, ikiwemo kuanzishwa kwa bidhaa mbalimbali za uwekezaji, yamepanua ushiriki wa wawekezaji sokoni.“Tumezindua bidhaa mpya sokoni, ikiwemo Exchange Traded Funds (ETFs), ili kuwapa wateja wetu wigo mpana zaidi wa chaguzi za uwekezaji.”

Amefafanua hatua hiyo  imechangia ongezeko la idadi ya wawekezaji binafsi wanaoshiriki katika soko la mitaji.

Kwa upande wake Meneja wa Utafiti na Uchambuzi kutoka Vertex International Securities Ltd Frank Abel amesema kampuni yao ilianzisha jukwaa hilo ili kuwaleta pamoja wadau wa soko la mitaji, kupitia kupitia mafanikio ya soko na kujadili maendeleo, ikiwemo uzinduzi wa bidhaa mpya kama ETFs.

Ambapo pia ameonesha kuridhishwa na mwenendo mzuri wa soko, huku akibainisha idadi ya wawekezaji imekuwa ikiongezeka kwa kasi.“Ongezeko hili haliko tu kwenye hisa bali pia katika uwekezaji wa pamoja kupitia mifuko ya uwekezaji.”

Aidha ameishukuru Serikali kwa kuunda mazingira mazuri na wezeshi yaliyowawezesha wawekezaji kushiriki kikamilifu katika soko.Kwasasa mtu yeyote anaweza kununua hisa kupitia simu ya mkononi, jambo linalorahisisha uwekezaji zaidi kuliko hapo awali.

Amewahiza Watanzania kuwekeza katika soko la hisa huku wakifanya shughuli zao za kila siku, ikiwemo kupitia mifuko ya uwekezaji wa pamoja na mifumo mingine ya uwekezaji.

Wakati huo huo Geoffrey Malauri ambaye ni Mwenyekiti TISEBA amesema  mwenendo wa soko la hisa unahamasisha, akibainisha kuanzishwa kwa bidhaa mbalimbali sokoni, ikiwemo mifuko ya pensheni.

Amesema ubunifu kupitia majukwaa ya kidijitali umechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uwekezaji wa rejareja.“Kwenye miaka miwili iliyopita, teknolojia ya simu imesaidia kuvutia wawekezaji wapya sokoni, hasa wawekezaji binafsi pamoja na taasisi.”

Hata hivyo amesema kupitia teknolojia ya simu, wawekezaji wanaweza kununua na kuuza hisa kutoka mahali popote walipo.Pia mazingira mazuri na wezeshi pia yamevutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza katika soko letu la mitaji.

Amewahimiza Watanzania kuchukua fursa ya mazingira haya rafiki kununua hisa au hati fungani za serikali, huku akiwahimiza wawekezaji wa ndani na nje kuchunguza fursa zilizopo katika masoko ya mitaji.

Pamoja na hayo ongezeko la bidhaa za kifedha sokoni, ikiwemo Exchange Traded Funds (ETFs), limechangia kuongeza uwekezaji katika masoko ya mitaji hapa nchini.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad