JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Benki ya Absa Tanzania yakabidhi zawadi ya fedha TZS Milioni 48, ikihitimisha Kampeni ya “Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa”

Share This
Benki ya Absa Tanzania imekabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni yake ya “Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa”, ikihitimisha kampeni yake ya miezi mitatu iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja na watanzania kutumia huduma za kibenki kwa njia za kidigitali katika kufanya miamala mbalimbali ya kifedha.

Katika hafla hiyo, mteja wa benki hiyo, Bi. Nasreen Karim Abdallah alikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 30, baada ya kuibuka mshindi wa droo kubwa iliyofanyika januari 21 mwaka huu, huku washindi wengine wa kila mwezi akiwemo Bw. Abdulrazak Ali Seif aliyepata TZS milioni 10, Bi. Aysha Mbarak Meghji aliyepata TZS milioni 5, na Bw. Gibbons Samuel Katule aliyepata TZS milioni 3 na wote kwa pamoja wakithibisha fedha hizo kuingizwa katika akaunti zao.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser alisema, kampeni hiyo ililenga katika kuwazawadia wateja wao kwa kuendelea kutumia huduma za kibenki zilizo salama, rahisi na za kisasa; “Zaidi ya zawadi, tunajivunia mabadiliko chanya tuliyoyaona kuelekea matumizi ya miamala isiyo ya fedha taslimu, ambayo huokoa muda, hupunguza hatari na kuchangia ujumuishi wa kifedha, hafla ya leo inaashiria mafanikio ya kampeni ambayo yamebadilisha maisha ya watu wengi.

“Dhamira yetu iko wazi, Kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja, hatua moja baada ya nyingine. Kila kampeni, kila ubunifu na kila zawadi tunayotoa inaongozwa na imani yetu kwamba Stori yako ina thamani”, alisema Bw. Laiser.

Kampeni hiyo ilionesha ongezeko kubwa la matumizi ya kadi na huduma za kidijitali, ikithibitisha mwelekeo unaokua wa wateja kupendelea huduma za kibenki zinazopatikana muda wowote na mahali popote, huku zikisaidia kupunguza foleni ndefu katika matawi na kuongeza kasi, usalama na urahisi wa huduma.

Akizungumzia mafanikio ya kampeni hiyo, Bi. Ndabu Swere alisema;

“Kampeni ya “Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa” inaonesha jinsi miamala midogo ya kila siku inavyoweza kuwa na nguvu kubwa. Wateja waliitikia vyema, wakidumu katika kufanya miamala kwa njia za kidijitali, na kwa upande wetu tuliweza kuwazawadia uaminifu wao kwa njia yenye maana.”

Kwa upande wake, mshindi wa zawadi kubwa, Bi. Nasreen Karim Abdallah, aliishukuru Benki ya Absa kwa zawadi hiyo, akisema ushindi huo ni hatua muhimu katika maisha yake. Alibainisha pia urahisi wa kushiriki kampeni hiyo kwa kutumia tu kadi katika miamala ya kila siku.

“Kilichonivutia zaidi ni urahisi wa kushiriki, ni kutumia tu kadi yangu kwenye matumizi ya kawaida. Zawadi hii haithibitishi tu umuhimu wa huduma za kidijitali katika maisha yetu ya kila siku, bali pia ni ya kubadilisha maisha,” alisema.

Benki ya Absa Tanzania imethibitisha dhamira yake ya kuendelea kubuni bidhaa na kampeni zinazowaletea wateja thamani zaidi, ikikumbusha kuwa mwaka 2024 benki hiyo ilitoa zawadi ya magari matatu na mwaka 2025 imetoa TZS milioni 120 kama zawadi za fedha taslimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akikabidhi mfano wa hundi ya shs 30,000,000 kwa mshindi wa droo kubwa ya kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ Bi.Nasreen Karim Abdallah (wa pili kushoto), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katika kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo na watanzania kutumia huduma za kibenki kwa njia za kidigitali, zawadi zenye jumla ya shs 120,000,000 zilitolewa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akizungumza katika hafla ambayo benki hiyo ilikabidhi mfano wa hundi ya shs 30,000,000 kwa mshindi wa droo kubwa ya kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ Bi.Nasreen Karim Abdallah (kushoto), jijini Dar es Salaam jana. Katika kampeni ya miezi mitatu iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo na watanzania kutumia huduma za kibenki kwa njia za kidigitali, zawadi zenye jumla ya shs 120,000,000 zilitolewa. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akikabidhi mfano wa hundi ya shs 3,000,000 kwa mmoja wa washindi wa droo ya kila mwezi ya kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ Bw. Gibbons Samuel Katule (wa pili kushoto), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katika kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo na watanzania kutumia huduma za kibenki kwa njia za kidigitali, zawadi zenye jumla ya shs 120,000,000 zilitolewa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akikabidhi mfano wa hundi ya shs 3,000,000 kwa mmoja wa washindi wa droo ya kila mwezi ya kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ Bw. Gibbons Samuel Katule (wa pili kushoto), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katika kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo na watanzania kutumia huduma za kibenki kwa njia za kidigitali, zawadi zenye jumla ya shs 120,000,000 zilitolewa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga.
Mshindi wa droo kubwa ya kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’, Bi. Nasreen Karim Abdallah (kushoto), akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya shs 30,000,000 jijini Dar es Salaam jana. Kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo na watanzania kutumia huduma za kibenki kwa njia za kidigitali, zawadi zenye jumla ya shs 120,000,000 zilitolewa. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad