JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAZIRI SANGU AWAAGIZA WENYE VIWANDA KUIMARISHA AFYA NA USALAMA WA WAFANYAKAZI

Share This



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, akizungumza na menejimenti na watumishi wa Kiwanda cha Omega Fish Limited (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa sheria ya Usalama naAfya Mahali pa Kazi na sheria nyingine za kazi katika kiwanda hicho Januari 5, 2026.


Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amewataka wamiliki wa viwanda na maeneo mengine ya kazi nchini kuzingatia kanunibora za usalama na afya ili kulinda guvukazi inayotumika katika uzalishaji viwandani.

Ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kufuatilia umadhubuti wa mifumo ya usalama naafya katika kiwanda cha kusindika samaki cha Omega Fish Limited cha Jijini Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi za kutembelea Taasisi na wadaumbalimbali wa sekta ya Kazi, Ajira na Mahusiano tangu alipoteuliwa kuiongoza Wizarayenye dhamana ya Masuala ya Kazi nchini.

Waziri Sangu amesema ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba nguvukazi ya nchiinayotumika kutimiza malengo yake hususan utekelezaji wa Dira ya Taifa ya mwaka2050, inalindwa kikamilifu na hivyo ameuelekeza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuwa karibu na kushirikiana na wawekezaji katika kusimika mifumomadhubuti ya usalama na afya mahali pa kazi.

“Kanda ya Ziwa ina shughuli nyingi za kiuchumi ukiachilia mbali sekta hii ya uvuviambayo OSHA mmeifanyia kazi nzuri ya ukaguzi kuna sekta nyingine kama vile sektaya madini ambako kuna baadhi ya migodi bubu inaanzishwa pasipo kufuata taratibu za usalama na afya,” ameeleza Waziri Sangu na kuongeza:

Hivyo, ninaiagiza OSHA kufanya ukaguzi wa kina kwenye maeneo ya kazi nchiniyakiwemo ya sekta ya madini ili kuhakikisha kunakuwa na uzingatiaji wa taratibu zotemuhimu za usalama na afya jambo ambalo ni muhimu katika kulinda afya za watu nakuongeza tija katika uzalishaji.”

Awali Katibu wa Jumuiya ya viwanda vya kusindika Samaki, Bw. Onesmo Sule, ambayealikuwepo katika ziara ya Waziri, ameeleza changamoto zinazowakabili wasindikaji wasamaki nchini zikiwemo upungufu wa malighafi unaosababishwa kwa kiwango kikubwana shughuli za uvuvi haramu na hivyo kupelekea viwanda kuzalisha chini ya uwezojambo linaloathiri ajira za watanzania pamoja na kupoteza mapato ya fedha za kigeni.

Aidha, changamoto hiyo ilielezwa katika risala ya kiwanda cha Omega Fish Limited iliyosomwa na Afisa Usimamizi Rasilimali Watu wa Kiwanada hicho, Bi. Zena Marijan Juma ambaye aliwasilisha risala hiyo mbele ya Waziri kwa niaba ya MkurugenziMtendaji wa kiwanda, Bw. Hamad Alsalman.

Akiongelea changamoto hizo za wadau Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano, amesemaserikali imezipokea changamoto za wadau wa sekta ya uvuvi kwa uzito mkubwaambapo ameeleza kuwa changamoto hizo zitashughulikiwa kwa ushirikiano baina yakena Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, ambayealiambatana na Waziri Sangu pamoja na watendaji wengine wa OSHA, amesema ziarahiyo ya Waziri imelenga kufuatilia utekelezaji wa sheria na kanuni za Usalama na Afya mahali pa kazi katika kiwanda hicho kwa mujibu wa miongozo ya OSHA.

“Ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku ya kufanya ukaguziwa mifumo ya usalama na afya katika maeneo mbalimbali ya kazi na kimsingi, tumeridhishwa na namna kiwanda hiki kinavyotekeleza miongozo ambayo tumekuwa tukiwapatia mara kwa mara,” ameeleza Kiongozi huyo Mkuu wa OSHA.

Kiwanda cha Omega Fish Limited ni miongoni mwa viwanda 64 vya kusindika samakinchini ambacho kinasindika samaki aina ya sangara na kuuza katika nchi mbalimbali za ulaya na bara la Asia.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Mifugo na Uvuvi, uvuvi ni sekta muhimu katikamaendeleo ya uchumi wa Taifa. Katika mwaka 2023, sekta ya uvuvi ilichangia asilimia1.7 kwenye Pato la Taifa (GDP) na kukua kwa asilimia 1.4. Aidha, sekta hii inatoa ajira kwa watanzania takriban milioni 6, zikiwemo ajira za moja kwa moja kwa wavuvi wapatao 201,661 na wakuzaji viumbe maji 49,084 katika mnyororo wa thamani.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, akizungumza na menejimenti na watumishi wa Kiwanda cha Omega Fish Limited (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa sheria ya Usalama naAfya Mahali pa Kazi na sheria nyingine za kazi katika kiwanda hicho Januari 5, 2026.Meza kuu ni Mkendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda, Bw. Hamad Alsalman (kushoto).




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, akitembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji katika kiwanda cha Omega Fish Limited akiwa ameambatana na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda, Bw. Hamad Alsalman, watendaji wa ofisi yake wakiwemo OSHA na wafanyakazi wa kiwanda cha Omega Fish Limited.



Wafanyakazi wa kiwanda cha Omega Fish Limited wakitekeleza majukumu yao ya kilasiku kiwandani.



Sehemu ya malighafi ya kiwanda cha Omega Fish Limited cha Jijini Mwanza ikiwakatika hatua tofauti za usindikaji.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti na watumishi wa Kiwanda cha Omega Fish Limited alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na sheria nyingine za kazi katika kiwanda hicho Januari 5, 2026.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano)alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na sheria nyingine za kazi katika Kiwanda cha Omega Fish Limited Januari 5, 2026.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na sheria nyingine za kazi katika Kiwanda cha Omega Fish Limited Januari 5, 2026.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad