JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Waziri Kombo Aagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China

Share This

 




Waziri Kombo Aagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameagana na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Wang Yi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Wang Yi alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia Januari 9-10 2026. Ziara hiyo ililenga kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa kihistoria na wa kimkakati kati ya Tanzania na China.

Akiwa nchini, Mheshimiwa Waziri Wang Yi alifanya mazungumzo ya uwili na mwenyeji wake Mheshimiwa Waziri Kombo na kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuagana, Mheshimiwa Waziri Kombo alimshukuru Mheshimiwa Waziri Wang Yi na ujumbe wake kwa kuichagua Tanzania kuwa sehemu ya ziara yake na kusisitiza kuwa ziara hiyo imezidi kuimarisha uhusiano wa kindugu, mshikamano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China.

Alisema ni matarajio ya Tanzania kuona makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara hiyo yakitekelezwa kwa vitendo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Naye Mheshimiwa Wang Yi ameiishukuru Serikali ya Tanzania kwa mapokezi na ukarimu alioupata wakati wa ziara yake na kueleza kuridhishwa na kiwango cha ushirikiano kilichopo na akaahidi kuwa China itaendelea kuwa mshirika wa karibu na wa kuaminika wa Tanzania katika juhudi zake za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad