JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Watanzania watakiwa kuwa makini na wapotoshaji katika mitandao-Mchange

Share This

 

Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI  wa kituo cha wanahabari watetezi wa rasilimali na taarifa – MECIRA, Habibu Mchange, amewataka Watanzania kuziangalia kwa macho makali kampeni za upotoshaji zinazofanywa mitandaoni zinazopelekea baadhi ya watu kutiwa hofu kiasi cha kukaribia kuamini uwongo unaosambazwa, ambao mara nyingi huendeshwa na akaunti bandia ni watanzania ambao wako ndani ya nchi na wengine wako nje nchi.

Akizungumza katika kipindi cha Kipima Joto kinachorushwa na ITV Ijumaa tarehe 9 Januari, 2026, Mchange alisema kuwa ukiingia mitandaoni utakachokiona na kinachoendelea unaweza ukafikiri nchi haipo au ina mapambano makali, wakati hali ilivyo mtaani na unayoyasoma ni vitu viwili tofauti kabisa akisisitiza kuwa kwa sasa wanasiasa wameacha kuweka nguvu katika kuwafikia wananchi ana kwa ana na badala yake wamehamishia nguvu zao mitandaoni.

Mchange alisema kuna watu hawalimi, hawafugi, hawafanyi kazi yoyote, lakini kutwa kucha wako mitandaoni kutukana, hao ndio wanaoonekana sana mitandaoni, wanapiga kelele, wanatukana na kushambulia, lakini hawaakisi hata kidogo uhalisia wa maisha ya Watanzania walio wengi.

Aliongeza kuwa mtaani hali ni tofauti kabisa, kwani watu wanakimbizana na maisha, wanatafuta riziki zao kwa amani, furaha na utulivu.

“Watu wanajibidiisha kila kukicha, kuhakikisha wanapata mkate wao wa siku, bila muda wa kupoteza kwenye makelele ya mitandaoni”. Amesema

Mchange anabainisha kuwepo kwa mkakati wa makusudi wa kutumia matusi ya mtandaoni kama mbinu ya siasa kupitia kaulimbiu ya “kupiga spana”, akieleza kuwa kaulimbiu hiyo imetumika kuhalalisha kutukana, kubeza na kushambulia watu wenye mawazo kinzani, huku wahusika wakidhani wanajenga ushawishi wa kisiasa.

Mchange aliisema michezo hiyo inaratibiwa kwa pamoja na wanamitandao ambao wamefungiwa Nairobi na nchi nyingine, wakilishwa, wakilipiwa makazi na familia zao kuhudumiwa ili kazi yao kubwa iwe ni kutengeneza hofu kwa jamii ya Watanzania waliopo ndani ya nchi kupitia uwongo na propaganda zinazosambazwa mitandaoni pamoja na wenzao waliopo ndani ya nchi

Amebainisha kuwa kelele nyingi za mitandaoni hazina uhusiano na maisha halisi ya wananchi, na kwamba mitandao imejaa sauti za watu wachache wasiokuwa kwenye uhalisia wa nchi wanayoizungumzia akisisitiza kuwa mitandao ya kijamii si kioo cha maisha ya Watanzania, na kwamba uhalisia wa maisha uko mtaani, mashambani na kwenye shughuli halali za kila siku za wananchi, si kwenye akaunti bandia, matusi na makelele yanayoendeshwa kwa maslahi ya watu wachache.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad