JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TASAC YAPOKEA BOTI YA UTAFUTAJI NA UOKOJI KIGOMA

Share This

 

Nahodha Grayson Marwa ni Mkaguzi Mwandamizi wa Meli Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi na  majaribio ya Boti ya Utafutaji na Uokoaji Mkoani Kigoma
Maafisa wa TASAC na Wazabuni wa Boti ya Utafutaji na Uokoji wakiwa ndani ya Boti mara baada ya kuifanyia majaribio Ziwa Tanganyika  mkoani Kigoma.


TASAC YAPOKEA BOTI YA UTAFUTAJI NA UOKOJI KIGOMA

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  limesema kuwa vyombo   vya utafutaji na uokozi kwa watumiaji wa vyombo usafiri  ni kipaumbele  katika kuimarisha usalama wa usafiri majini katika Ziwa Tanganyika.

Hayo ameyasema Nahodha Gryson Marwa, Afisa Mwandamizi wa Ukaguzi na Usajili wa Meli kutoka (TASAC) wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukaguzi, majaribio na mapokezi rasmi ya boti ya utafutaji na uokoaji (SAR – TASAC II) katika Bandari ya Kigoma.


Marwa ameongeza kuwa TASAC inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha ununuzi wa boti tano za utafutaji na uokoaji ikiwemo na 
 Mkoa wa Kigoma kupata boti moja katika kuongeza ufanisi wa utoaji msaada  pale dharura za majini zinapotokea.

 Marwa amesema boti hiyo imepokelewa na kukaguliwa na  kuona imekidhi vigezo vilivyokuwa vinatakiwa. 

Hata hivyo amesema kuwa  boti hiyo ilianza kukaguliwa tangu ilipoanza kutengenezwa, na majaribio ni uthibitisho wa kiufundi kabla ya kuanza kutumika rasmi katika maji ya Ziwa Tanganyika.

“Mwendelezo huu ni dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika  kutekeleza kwa  vitendo maombi ya mahitaji ya wananchi. 

Amesema boti hiyo  itaongeza usalama na kupunguza madhara ya ajali ya usafiri majini kwa kuhakikisha msaada unapatikana kwa haraka.


Kwa upande wake, Nahodha Adam Mamiro, Afisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Kigoma, amempongeza  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Boti ya Utafuataji na Uokoaji  kwa Mkoa wa Kigoma katika kurahisisha na kuharakisha operesheni za utafutaji na uokoaji kwa wavuvi na wasafiri wa Ziwa Tanganyika.


Nahodha Mamiro amesema Boti hiyo itahudumia maeneo ya jirani ya Katavi na Rukwa huku  watumiaji wa vyombo vya majini wanapaswa kuendelea kuzingatia matumizi ya vifaa vya uokozi kama sehemu ya tahadhari binafsi.

Mvuvi wa mwalo wa Kigodeko Choba Aiseni  wameishukuru Serikali kwa uwekezaji huo wakisema hapo awali walikumbana na changamoto kubwa ya kuokolewa kwa wakati, hasa wakati wa upepo mkali wa Kaskazi, Nyamori na Sabasaba.

“Kwa kupata boti hii tumefurahi sana kuona boti hii, sasa tuna uhakika kuwa msaada utapatikana kwa haraka tunapokumbwa na dharura majini,” amesema Aiseni.





Matukio mbalimbali ya majaribio ya Boti ya Utafutaji na Ukoaji Ziwa Tanganyika  mkoani Kigoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad