JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SERIKALI KUIFUNGUA PEMBA KIUTALII

Share This

 




Na. Mwandishi wetu, Pemba
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania, Mh. Hamad Hassan Chande (Mb), amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kushirikiana katika kuimarisha na kuendeleza sekta ya utalii ili kuchochea maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla

Mhe. Chande amebainisha hayo wakati wa uzinduzi wa Bonanza la Sita la Utalii wa Michezo na Utamaduni Pemba (Tamasha la Pemba Tourisport & Cultural Bonanza 2026) linalolenga kukifungua Kisiwa cha Pemba kiutalii, kuvutia wawekezaji, watalii wa ndani na nje ya nchi kwa kutangaza vivutio vilivyomo kwenye kisiwa hicho.

“Katika siku hizi nne ambazo tamasha hili linaendelea, ikiwa leo ni siku ya mwanzo naamini, watanzania, wenyeji na wageni watanufaika kuona vivutio mbalimbali ambavyo vitatangazwa na wataalamu wetu na kushawishika katika kuongezeka kwa wageni nje ya nchi, na ambao wamekuja mara moja niwaombe sana waje kwa mara ya pili, ya tatu na ya nne” alisema Mhe. Chande

Mhe. Chande, licha ya kuipongeza Kamisheni ya utalii pia ametoa wito kutangaza mazao mapya ya utalii yaliyopo kwenye Kisiwa hicho kwa ubunifu mkubwa kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza na kuongeza pato la taifa kupitia rasilimali zilizopo kwenye kisiwa hicho badala ya kuwa sehemu tu ya kutembelea

Mhe. Chande ameongeza kuwa, moja ya faida kubwa ya tamasha hilo ni kuwapatia vijana jukwaa la kuonesha uwezo wao katika fani mbalimbali ikiwemo michezo, sanaa na utamaduni ikiwa ni nafasi muhimu kwao katika kujiimarisha, kuingia kwenye masoko ya ajira, ubunifu, na kuonesha biashara zao.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Adil George, amesema kuendelea kufanyika kwa bonanza hilo ni utekelezaji wa maelekezo na shabaha ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ya kuleta mageuzi ya kiuchumi katika Kisiwa cha Pemba kupitia sekta ya utalii, michezo na utamaduni.

Bonanza la Utalii wa Michezo na Utamaduni Pemba linatarajiwa kuendelea kuwa chachu ya kuitangaza Pemba, kuimarisha mshikamano wa jamii na kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika uchumi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad