JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Furahika Kutatua Tatizo la Ajira Kwa Wale Wasio na Ujuzi

Share This

 


Na Mwandishi Wetu
CHUO cha Maendeleo ya Ujuzi na Viwanda Tawi la VETA Furahika Mbagala kimesema kuwa katika Maendeleo ya Viwanda nchini kunahitaji uzalishaji wa rasilimali watu yenye ujuzi wa kuhudumia viwanda hivyo.

Akizungumza na Michuzi Media Mkurugenzi wa VETA Furahika David Msuya amesema Chuo hicho kimeanzishwa mahususi kwa ajili ya vijana kupata ujuzi bila malipo.

Amesema kuwa vijana wanakosa sifa za kuajiriwa kutokana na kutokuwa na ujuzi huvyo chuo cha maendeleo kimefungua mlango

Msuya amesema kuwa kuwa serikali ya awamu sita imeweza kuvutia uwekezaji wa viwanda hivyo kunahitaji rasilimali yenye ujuzi.

Aidha amesema kuwa kozi zinazopatikana katika chuo hicho zinaendana na mazingira ya sasa ya mapinduzi teknolojia.

Amesema kuwa wataendelea kutoa elimu bure ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi ili weweze kujitegemea na kuongeza ajira.

Kozi hizo ni Hoteli kwa miezi 6 na Mwaka ,Usafi wa Maofisini na Mawakala wa Forodha ,Ushonaji ,Computer,Utalii ,Urembo ,Udeereva,Ufundi wa Magari ,Useremala ,Ualimu wa Awali ,Makatibu Muhtasi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad