JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WIZARA YA KILIMO YADHAMIRIA KUWATUMIA WAHITIMU WA MoCU KATIKA MIRADI YA BBT

Share This

 









Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Stephen Nindi amewataka wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kutumia ipasavyo elimu na ujuzi walioupata katika kuchangia maendeleo ya Sekta ya Kilimo na uchumi wa nchi kupitia programu ya vijana ya Building a Better Tomorrow (BBT).

Dkt. Nindi amesema hayo wakati akimwakilisha Bw. Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo katika Mahafali ya 11 ya MoCU tarehe 11 Desemba 2025 ambapo alikuwa mgeni rasmi katika kutoa tuzo na zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika ngazi mbalimbali za kitaaluma, michezo na uongozi kwa mwaka 2025. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa J.K. Nyerere, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hizo, Dkt. Nindi amewasisitizia wahitimu kutumia maarifa yao kwa vitendo kwa kushirikiana na wataalamu waliopo kwenye Sekta tofauti za uzalishaji hususan kilimo, ili kuongeza ufanisi, ubunifu na tija kwenye maeneo watakayotoa hudumia.

Dkt. Nindi pia ameahidi kuimarisha ushirikiano na MoCU ikiwemo kutoa tuzo maalum za pamoja kwa washindi mbalimbali. Hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za Chuo hicho katika kuhamasisha ushindani chanya na ubora katika taaluma, uongozi na ubunifu miongoni mwa wanafunzi.

Ushirikiano huo utatoa fursa kwa wahitimu wengi zaidi kushiriki moja kwa moja katika miradi ya maendeleo ikiwemo programu ya BBT, hivyo kusaidia kupata wataalamu vijana watakaoleta mageuzi kwenye Sekta ya Kilimo nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad