WIZARA ya Afya imesikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu wenye nia ovu ambao wamekuwa wakitumia jina la Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa kuwatapeli watu kwamba anaozesha mwanae, hivyo kuwaomba michango ya harusi ya mtoto wa Mhe. Mchengerwa.
Tunapenda kutoa taarifa kuwa, Mhe. Mchengerwa hana mtototo anayemuozesha na kwamba hajawahi kumtuma mtu yoyote kuomba michango kwa ajili ya harusi yoyote.
Wizara ya Afya inapenda kutoa onyo kwa yoyote anayejihusisha na vitendo hivyo vya uvunjaji wa sheria na kwamba tayari imeshatoa taarifa kwenye mamlaka husika kuhusu namba zote zinazotumika kwa hatua za kisheria.
Aidha, Wizara inatoa wito kwa viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuwapuuza matapeli hao.
Imetolewa na;
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI



No comments:
Post a Comment