
Na John Mapepele, New Delhi
Waziri wa Afya wa Tanzania, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa amewasili New Delhi, nchini India, tayari leo kushiriki Mkutano wa pili wa Kimataifa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu tiba asili ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Tanzania katika kushirikiana na mataifa mbalimbali kwenye kuboresha huduma ya afya kwa wananchi ambapo amepokelewa na ujumbe wa ubalozi wa Tanzania India ukiongozwa na Mhe. Balozi, Anisa Mbega.
Mkutano huu wa kimataifa unaoratibiwa moja kwa moja WHO kwa kushirikiana na Serikali ya India unajumuisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wasimamizi wakuu wa sekta ya afya katika nchi mbalimbali hususan mawaziri watunga sera wakuu, na wataalam wa fani tofauti lengo likiwa ni kujadili nafasi ya tiba asili katika kuimarisha mifumo ya huduma za afya.

Akiongea mara baada ya kuwasili jijini New Delhi, Mhe. Mchengerwa amesema miongoni mwa mambo makubwa yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na utawala na udhibiti wa tiba asili, utafiti na Ushahidi wa kisayansi, ujumuishaji wa tiba asili katika mifumo ya afya, matumizi endelevu ya raslimali za kiasili, uendelezaji wa raslimali watu, pamoja na ushirikiano wa kimataifa sambamba na mkakati wa WHO wa Tiba qhTanzania katika mkutano huo katika kipindi hiki unaonesha dhamira ya Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tiba asili inaendeshwa kwa kuzinngatia, Ushahidi wa kisayansi, usalama na mifumo madhubuti ya udhibiti kama sehemu za kuimarisha huduma za afya, na kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma ya afya kwa wote nchini.
Pia hivi karibuni wakati wa kikao kazi na wafanyakazi wa Taifa ya Muhimbili Mhe Mchengerwa alitoa dira ya Wizara yake huku akiainisha maeneo sita ya mageuzi yanayolenga kuipeleka Sekta ya Afya katika viwango vya juu ili kuwakomboa wananchi kwenye eneo la afya huku akipigia msumari wa moto maelekezo mahususi ya Mhe. Rais Samia ya kuanzisha Bima ya Afya kwa wote, kuhakikisha wagonjwa wasio na uwezo wanaendelea kupatiwa huduma zote za afya bila kikwazo cha fedha, pia hospitali zote nchini zinaacha mara moja kuzuia maiti kwa sababu za kudaiwa gharama za matibabu.

Kando ya mkutano huo, ubalozi wa Tanzania nchini India umeandaa mikutano na vikao vya mazungumzo vinavyolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya kati ya Tanzania na India, ikiwa ni pamoja na utaratibu wa usainiwaji wa hati ya makubaliano (MoU) kuhusu ushirikiano katika mfumo wa tiba asili ya Ayurveda ya India kati ya Wizara ya AYUSH ya Serikali ya India na Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



No comments:
Post a Comment