JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Wadau Wakutana Kujadili Ufanisi na Uendelevu wa Bandari

Share This

Na Mwandishi wetu ,Dar es Salaam

WADAU zaidi ya 100 kutoka taasisi za serikali, mamlaka za bandari na usafiri, sekta binafsi ya usafirishaji, waagizaji, wauzaji nje na wamiliki wa mizigo wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili ufanisi wa bandari na uendelevu wa uendeshaji wake kupitia ushirikiano wa sekta ya Umma na binafsi (PPP).

 Mkutano huo wa majadiliano ya pamoja kati ya sekta ya umma na binafsi umelenga kubaini changamoto za biashara na usafirishaji katika bandari za Tanzania, kujadili suluhisho za vitendo kupitia ushirikiano wa sekta hizo mbili, pamoja na kuangalia namna ya kuwezesha biashara na kuendeleza miundombinu ya bandari.

Mada kuu ya mjadala huo ilikuwa “Kuendesha Operesheni Endelevu za Bandari Kupitia Ushirikiano wa Umma na Binafsi.”
Akifungua mjadala huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ushirikiano wa Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila, amesema sekta ya bandari na usafirishaji ni nguzo muhimu ya uchumi wa Taifa na ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi endapo itawekewa uwekezaji wa kutosha.
 Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeamua kuingiza sekta binafsi katika kutafuta na kutekeleza suluhisho la changamoto za kiuchumi kupitia miradi ya PPP, hatua inayolenga kuongeza mtaji, ufanisi na teknolojia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia, aliyekuwa mchokoza mada kuhusu matumizi ya PPP katika maendeleo ya miundombinu ya biashara, alisema ni muhimu kwa sekta za kimkakati kumilikiwa, kudhibitiwa na kuendeshwa na Watanzania.

Amesisitiza umuhimu wa kuzingatia sera ya local content kwa kuwapa Watanzania kipaumbele katika miradi ya kimkakati, ikiwemo kuweka masharti kwa wawekezaji kuhakikisha asilimia fulani ya umiliki na ushiriki inakuwa ya wazawa.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad