JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TASAC YANUNUA BOTI MBILI ZA UTAFUTAJI NA UKOAJI TANGA NA KIGOMA

Share This

 Muonekano wa boti mbili za Utafutaji na Uokozi zinazokwenda kutoa huduma Ziwa Tanganyika na Tanga.

Kaimu Meneja wa Usajili na Ukaguzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mhandisi Said Kaheneko akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na ujio wa Boti mbili za Kisasa za Uokoaji zilizoundwa nchni Uturuki zitakwenda katika kuhudumia Bahari ya Tanga pamoja Ziwa Tanganyika Kigoma ,jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limenunua Boti Mbili za Kisasa Nchini Uturuki kwa ajili Utafutaji na Uokoaji wananchi wanaofanya shughuli za Uvuvi na Usafirisaji wa Abiria katika Bandari ya Tanga na Ziwa Tanganyika Kigoma.

Boti hizo zimetokana na mapato ya Shirika hilo hilo katika kutatua changamoto za utafutaji na uokoaji pindi vyombo vya majini vinapokuwa vimepata majanga ya kuzama au kupoteza mwelekeo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Usajili na Ukaguzi wa TASAC Mhandisi Said Kaheneko amesema kuwa hiyo hatua ni mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wanaofanya biashara katika maziwa na bahari wanapata huduma za ukuoji pindi wanapopata majanga katika vyombo vyao.

Amesema kuwa boti hizo ni za kisasa zinaweza kwenda kwa spidi pundi wakipata taarifa kuhusiana na chombo cha majini kuzama au kupoteza mwelekeo.

Aidha amesema Shirika linathamini uchumi wa wananchi katika bahari na Maziwa kuwa na uhakika wa kupata huduma uokozi pundi panapotokea majanga mbalimbali katika safari za vyombo vya majini.

Hata hivyo amesema kuwa wataendelea kununua boti hizo katika kila maeneo ili kuendelea kulinda wananchi wanaofanya biashara na usafiri katika usafiri wa maji.

Mhandisi Kaheneko amesema kuwa kwa upande wa Kigoma itasaidia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na mwingiliano wa Ziwa Ziwa Tanganyika.

Amesema kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu( Red Cross) takwimu zinaonyesha watu 5000 hufariki dunia katika vyombo vya majini hivyo uwekezaji wa vyombo vya utafutaji na uokaji itakwenda kupunguza idadi vifo hivyo.

Nae Mkaguzi Mwandamizi wa Vyombo vya Ndani na Nje ya Nchi wa TASAC Grayson Marwa amesema Boti hizo wamezifanyia ukaguzi wa kina tangu kuundwa kwake hadi kukamilika.

Amesema kuwa boti hizo zina uwezo wa kwenda mbali kwa muda mfupi hali ambayo suala la uukoji utakuwa rahisi.

Meneja wa Usalama wa Kampuni ya Raphael Logistics Denis Mrema amesema kuwa usafirishaji wa boti hizo kwa Tanga ni siku mbili na Kigoma katika Ziwa Tanganyika siku Tatu kutokana na walivyojipanga katika usafirishaji boti hizo.

Amesema kuwa kampuni hiyo wanauzoefu wa usafirishaji wa mizigo mikubwa na kuamini boti hizo zitafika salama.
Meneja wa Usalama wa Kampuni ya Raphael Logistics Denis Mrema akizungumza kuhusiana usafirishaji wa Boti hizo katika Ziwa Tanganyika na Tanga ,jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Mwandamizi wa Vyombo vya Ndani na Nje ya Nchi wa TASAC Nahodha Grayson Marwa akitoa maelezo kuhusiana boti boti zitavvyofanya kazi katika shughuli za Utafutaji na Uokoji katika Ziwa Tanganyika pamoja na Pamoja na Tanga.

Picha ya pamoja wa Maafisa wa TASAC mara baada ya ukaguzi wa Boti za Utafutaji na Uokozi kwa ajili ya kuanza Safari ya Tanga na Kigoma .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad