Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imepewa tuzo ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya sekta ya uchukuzi nchini.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Mkude akimwakilisha Waziri wa Uchukuzi na kupokelewa na Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu, Mhandisi Edward Amboka.
Tuzo hiyo imetolewa katika Mkutano wa 18 wa Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
TARURA imeshiriki Mkutano huo ikiwa ni mdau wa sekta ya uchukuzi, ambapo ilitumia Mkutano huo kwa kuwasilisha utekelezaji wa shughuli za Wakala kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kutoa elimu kwa wadau kuhusu majukumu na kazi mbalimbali zinazofanywa na Wakala.


No comments:
Post a Comment