JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TANZANIA YAUNGA MKONO UENDELEVU WA BONDE LA NILE

Share This

  


TANZANIA YAUNGA MKONO UENDELEVU WA BONDE LA NILE

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitisha kuendelea kulisaidia Bonde la Mto Nile, ikisisitiza kuwa Tanzania inatambua thamani kubwa ya rasilimali maji katika bonde hilo na umuhimu wa usimamizi shirikishi kwa maendeleo ya nchi wanachama.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika tarehe 06 Disemba, 2025 jijini Bujumbura nchini Burundi, Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Andrea Mathew amesema kizazi cha sasa kina wajibu wa kuhakikisha Mto Nile unaendelea kutiririka kwa manufaa ya nchi zote zinazoutegemea, akisisitiza umuhimu wa majadiliano endelevu na ushirikiano wa kikanda.

Mhandisi Kundo amesema mipango ya pamoja ya usimamizi shirikishi wa rasilimali za maji ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa maji na kuimarisha mahusiano ya Kimataifa, akiongeza kuwa kufanya kazi kwa kutengana ni mtazamo uliopitwa na wakati.

Pia, Mhandisi Kundo amesisitiza umuhimu wa nchi wanachama kutimiza wajibu wao wa kulipa michango inayoiwezesha taasisi hiyo kufanya kazi zake ipasavyo, akisema ulinganifu wa mchango wa kifedha ni chachu ya uendelevu wa miradi katika Bonde la Nile.

Hata hivyo Mhandisi Kundo amesema ili Bonde hili liendelee kuwa na tija, mataifa yote yanapaswa kuimarisha mshikamano, kushirikiana katika kutatua changamoto na kuhakikisha matumizi ya rasilimali maji yanazingatia usawa, haki na uwajibikaji.






 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad