WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amezindua Miongozo ya Uzalishaji Endelevu wa Mazao ya Ufuta na Jamii ya Mikunde tarehe 12 Desemba 2025 mkoani Lindi na kuwataka Maafisa Ugani na Maafisa Ushirika kutoa elimu kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wenye tija na kufikia masoko kwa faida. Miongozo hiyo ni ya mazao ya Choroko, Mbaazi, Maharage, Soya na Ufuta.
“Nyinyi ni mabega ya Sekta ya Kilimo kwa kubeba jukumu la kutoa elimu na kuwashauri wakulima kuhusu teknolojia na mbinu bora za uzalishaji kwa kuongeza uzalishaji wenye tija na endelevui ili kufikia masoko kwa faida,” amesema Waziri Chongolo. Ameongeza kuwa wakulima ndiyo msingi wa ujenzi wa uchumi wa viwanda na ustawi wa jamii zeru.
Waziri Chongolo amepongeza hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Zainab Telack kuwakutanisha zaidi ya wataalamu 600 kitendo ambacho kinaomesha dhamira ya dhati ya Mkoa ya kujielekeza kutafuta tija kwenye kilimo.
Ameipongeza pia Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), kwa kutekeleza hatua za kuwa na mpango wa kusambaza mbegu bora kwa wakulima; mpango wa kuchagiza huduma za ugani chini ya halmashauri na vijana wa BBT; na mpango wa utekelezaji wa viwango endelevu na viwango bora vya uzalishaji.
Waziri Chongolo ameeleza kuwa COPRA imengia mikataba na Bodi ya Korosho katika kuhakikisha vijana wa BBT wanasimamia mazao ya ufuta na jamii ya mikunde ili wakulima waongeze uzalishaji wenye tija kwa mazao yao.
“Mwezi Julai 2026 tunajipanga kuanzisha Wakala wa Huduma za Ugani ili kuongeza uzalishaji endelevu na salama na yenye viwango vyenye ubora,” amesema Waziri Chongolo.
Mkoa wa Lindi umedhamiria kuongeza wigo wa kilimo cha mazao mengine yakiwemo mboga mboga na matunda ili kuongeza fursa za ajira za kilimo biashara kwa wana-Lindi. Mazao yanayolimwa mkoani Lindi kwa saaa ni mbaazi, ufuta, minazi na korosho.


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)




No comments:
Post a Comment