*Asisitiza yeye haongozi Serikali ya wanyonge bali anaongoza Watanzania kuelekea Tanzania tunayoitaka
Na said Mwishehe,Michuzi TV-Iringa
MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewashukuru maelfu ya wananchi wa Iringa Vijijini kujitokeza kwa wingi katika mkutano wake wa kampeni kuelekea Oktoba 29 ,2025 huku akitumia nafasi hiyo kueleza wazi yeye anaongoza Serikali inayogusa maisha ya wananchi wq chini na wala haongozi Serikali ya wanyonge.
Akihutubia maelfu ya wananchi hao katika mkutano wake wa kampeni ,Mgombea Urais Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kueleza jambo moja kwamba ambalo yeye haongozi wanyonge bali anaongoza watanzania ambao anataka kuwajengea Tanzania tunayoitaka
“Nilisema nilipozungumza na wazee pale Dodoma ambapo nilliita wazee wote wa mikoa ushiriki wao ulikuja nilizungumza nao jambo moja kubwa ambalo nataka nilirudie hapa baada ya kusikiliza yaliyofanywa kuanzia nimeanza kampeni nilizindu Dar es Salaam baadae nikapita Morogoro, Songwe, Mbeya ,Njombe na leo nimefika Iringa
“Lakini mambo yote yanayozungumzwa ni mambo yaliyogusa mwananchi wa kule chini ndiye niliyemgusa sasa kuna maneno walikuwa wanasema hii Serikali siyo ya wanyonge na mimi niliwajibu mimi siongozi wanyonge mimi naongoza watanzania ambao nataka kuwajengea Tanzania tunayoitaka
“Sasa kwa yote yaliyosemwa na yatakayoendelea kusemwa yale mambo yamemgusa Mtanzania wa chini kabisa .Umeme uko vijijini unakwenda kwenye vitongoji,maji yanachotwa kwenye bomba kule vijijini , zahanati,vituo vya afya na vipimo vya maana viko wilayani na kwenye kata kwa wananchi.
“Lakini katika sekta ya elimu mashule mazuri yamejengwa vijijini.Nilipopita Songwe wakaniambia sisi ndio Mkoa peke yake tuna shule za msingi za ghorofa inamaana mtoto wa mkulima anakwenda kusoma kwenye ghorofa lenye mapanga boi mafeni yanampepea lakini madirisha ya vioo sasa huko ndio kumjali mnyonge.
“Na sio lazıma usimame mimi nina Serikali ya wanyonge hapana kumjali mnyonge ni kumfanyia hayo yakamgusa kule chini.Kwahiyo nilikuwa nataka niseme hilo na ndugu zangu na wazee wenzangu mnielewe,”amesema Dk.Samia mbele ya wananchi hao wa Iringa Vijijini.
Ameongeza hivyo kwa Serikali hiyo ya Chama Cha Mapinduzi kazi yao ni kuwafanyia kazi Watanznaia wa hali ya chini ili wanyanyuke waende nao pamoja kwenye uchumi jumuishi.”Huko ndio iko tunakoelekea.”
Awali wakati akianza kuzungumza na wananchi hao Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewashukuru kwa kujitokeza katika mkutano huo na kote ambako amepita maelfu ya wananchi wamejitokeza.
“Chifu Adamu Abdull Mkwawa Junior ahsante sana na himaya yako iliyopo hapa , natambua uwepo wenu Chifu mkubwa nimekuja leo nimefurahi kuwaona ahsanteni.
“Nimefurahi kufika hapa kwa Chifu Mkwawa na kukaribishwa na Chifu Adam Mkwawa Junior ,nimefutahi sana kupata baraka za kichifu wa hapa Kalenga.Mimi naitwa Chifu Hangaya ,ni Chifu mkubwa Tanzania lakini nilikuwa sijafika hapa kupata baraka za Chifu Mkwawa leo nimefurahi sana
“Nimefurahi kuona na ndugu zangu Wana wa Mkwawa wanaosifa kwa ujasiri na hali yao ya kupambana sasa mipango yetu ni kujenga taifa lenye uchumi jumuishi linalojitegemea kiuchumi na lenye ustawi ndio sababu ya kuja hapa kwenu kwa Wana Mkwawa kuomba kura zenu ili kwa pamoja tuingie kwa pamoja kuijenga Tanzania tunayoitaka.”
Mgombea Urais akiendelea kuzungumza na maelfu ya wananchi hao amesema anawashukuru kwa upendo na ukarimu kwa mapokezi makubwa waliyomuonesha.“Ahsanteni sana…
“Nimewasikiliza vema risala au maneno au hotuba za wabunge wenu wawili ndugu yangu Jackson Kiswaga wa Kalenga na kaka William Lukuvi wa Isman ,nimewasikiliza vizuri sana nimesikiliza mambo yote waliyosema yamefanywa hapa.”














No comments:
Post a Comment