JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ALICHOKISEMA MGOMBEA URAIS CCM DK.SAMIA KWA MAELFU YA WANANCHI MKOANI IRINGA

Share This

 *Akumbusba ahadi zake na jinsi zilivyotekelezwa ikiwemo miradi ya umwagiliaji, huduma za kijamii

*Aahidi kuendelea na ujenzi miundombinu ya barabara za lami, Kokoto maeneo mbalimbali 

*Akoshwa  na wananchi mikoa ya nyanda za juu kusini …Iringa leo mmefunika  Iringa …mna Vibe


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Iringa

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara zake kwa mikoa ya nyandq za juu kusini kwa kuhutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Iringa huku akitumia nafasi hiyo kueleza masuala mbalimbali yatakayokwenda kutekeleza miaka mitano ijayo.

Dk.Samia baada ya kuzindua kampeni zake mkoani Dar es Salaam alienda Morogoro kisha akaenda Mkoa wa Songwe kisha Mbeya,Njombe na leo Septemba 7,2025 amehitimisha kampeni katika mikoa ya nyandq za juu Kusini mkoani Iringa.

Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Iringa Mgombea Urais Dk.Samia amesema kote ambako amepita amekuwa akipokelewa na maelfu ya wananchi tena walio na Vibe(Shabgwe) la kutosha.

“Na kwa Mkoa wa Iringa siyo kwa wingi huu na kwa vibe hili, wengine wanawatizama wajipangeje wawapiku lakini mmetisha sana wana iringa.Katika safari hii tumesikia mengi yaliyofanywa na ambayo tumepanga kuyatekeleza. Katika hayo nikiwa hapa Iringa  mjini nataka kusema machache.

“Nilipofanya ziara ndani ya mkoa huu Agosti mwaka 2022 kuna mambo niliahidi na miongoni mwa hayo niliahidi tutaleta skimu za umwagiliaji tayari tumetekeleza miradi mbalimbali ya umwagiliaji maji ikiwemo miradi tisa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yenye thamani ya Sh.bilioni 104.4 na kuwanufaisha wakulima 64800.”

Ameongeza kuwa wamefanya mradi wa umwagiliaji maji wa Mtula uliopo mji wa Mafinga uliojengwa kwa fedha Sh.milioni 566. Mradi huo  umewezeaha shughuli za kilimo kuendelea kwa muda wote.

Amesema kuwa jitihada hizo zote zinalenga kuwezesha wakulima kuzalisha na kunufaika zaidi na kilimo wanachokifanya huku akisisitiza Serikali  imeendelea kununua pembejeo na mbolea kwa ruzuku ambayo imewezesha wakulima kuzalisha kwa wingi.

“Nikitolea mfano zao la kahawa uzalishaji umeongeza kutoka tani 109 mwaka 2020 hadi tani zaidi ya 300.Tumeweza kukuza uzalishaji wa mazao lakini kwa upande wa mahindi kutokana na pembejeo hizi na mbolea ya ruzuku…

“Mwaka huu Tanzania tumekuwa wa pili kwa  uzalishaji mahindi Afrika. Tumezalisha tani milioni 10.Mbolea hizi na pembejeo za ruzuku zinakuza kilimo kwa kiasi kikubwa.

“Hivyo basi mkituparidhaa tutaendelea kutoa  ruzuku ya mbolea kote nchini pamoja na pembejeo,  pia tutajenga vituo 50 vya kuhifadhia mazao ya parachichi, tutajenga vituo vingine vya baridi kuhifadhia mazao ya mbogamboga.

“Pia tutajenga maghala ya kuhifadhia mazao ya chakula na biashara na tutaanzisha vituo vya ukodishaji zana za kilimo ili wakulima waweze kupata huduma za kilimo kwa bei nafuu,”amesema Dk.Samia na kusisitiza vituo hivyo  bei yake  itakuwa nusu ya bei inayotozwa na sekta binafsi. 

Kuhusu sekta ya nishati amesema kuwa aliahidi kufikisha  miundombinu ya umeme kwenye vijiji vyote 360 vya mkoa wa Iringa.Tumefanya  hivyo na kazi inayoendelea sasa ni kupeleka umeme kwenye vitongoji kazi inaendelea vizuri.

“Vitongoji vingi tayari vimepata umeme na kazi inaendelea kwa hapa Iringa mjini tumefikisha umeme kwenye mitaa yote 189 kati ya 192 na ile michache iliyobaki wakandarasi wapo wanaendelea na kazi.

“Pamoja na kusambaza umeme Tanzania  nzima mijini, vijiini na vitongoji tunakazi ya kuongeza uzalishaji umeme ili uwe wa kutosha.Tumetoka megawati 1600 mwaka 2020 na mpaka mwaka huu tupo megawati 400

“Sasa tunajipanga kufikisha megawti 8000 kwa kutumia vyanzo mbalimbali anuwai ikiwemo upepo na jotoardhi ambao ukanda huu tunategemea kupata umeme mwingi wa upepo lakini na joto ardhi.Tunajipanga vyema ili umeme uwe ndiyo msingi au kichocheo cha maendeleo ya nchi yetu.

Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema ahadi nyingine aliyoitaa kwa wana Iringa  ilikuwa kuboresha kiwanja cha ndege Nduli ,sasa hivi mashirika kadhaa yanatoa huduma na Air Tanzania inaingia na kutoka Iringa.

“Wakati ule tuliahidi barabara ya mchepuko kupunguza msongamano ndani ya mji ujenzi huo umefikia asilimia 5 na fedha yote ya mradi imeshatoka na ujenzi unaendelea na ninaahidi  barabara itakamilika.

“Ahadi ya daraja la Kitwilu hadi Isakuliko daraja hili tumeliweka katika mpango wa TACTIC na mtakapotupa ridhaa mradi huo utakwenda kujenda daraja hili.Kwenye sekta ya miundombinu nimepokea maombi mengi ndani ya mkoa huu hata mikoa mingine niliyopita.

“Kwa kawaida kila safari moja ya maendeleo huanzisha nyingine ukijenga barabara moja ya lami watu wakionja raha ya lami wanadai na nyingine,”amesema Rais Dk.Samia.

Akifafanua amesema  ujenzi wa kilometa moja ni sawa na Sh.bilioni 1.2 ambayo ni kama vituo viwili vya afya. “Lakini hatutaacha, tutaendelea kujenga barabara za lami na  barabara za kokoto zipitike muda wote na tutafungua pia barabara nyingine na kila miaka inavyokwenda tutaendelea kujenga barabara.

Akizungumzia wafanyabiashara ndogondogo wa Mkoa wa Iringa amesema wakati ule aliahidi kujenga soko la machinga ,hivyo amewaambia eneo limeshatengwa ambalo lilikuwa stendi ya mabasi na sasa wameanza  taratibu za kutafuta fedha kujenga machinga complex ndani ya mji wa Iringa.

“Nataka niwaambie hili la  ahadi lengo langu nimalize kabla sijamaliza muda wangu wa kazi. Nataka nimalize machinga complex ndani ya Iringa na wanangu wamachinga na mama lishe na wengine wote waweze kufanya biashara zao.

“Manispaa imejenga ofisi ya machinga ,niliahidi nitatoa fedha kujenga ofisi za machinga mkoa yote nchini.Nilitoa fungu la fedha TAMISEMI  wakajazia zikaenda halmashauri wakasimamia ujenzi na ninaambiwa ofisi imejengwa inayowawezesha kuratibu kazi zao vizuri.”

Pamoja na hayo Dk.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia dhamira yao  kuwaboreshea mazingira ya kufanya biashara zao atakwenda.” “Nitakwenda kufanya hivyo hivyo. 

“Mbali na hayo tumechukua hatua mbalimbali kuboresha huduma za kijamii, maeneo ya elimu, afya, maji tumefanya vizuri sana miaka minne mitano iliyopita.

“Katika kukuza uchumi na ajira kwa vijana mkoa wa Iringa umeongeza viwanda wakati naingia ulikuwa na viwanda 24 vikubwa na sasa vipo 40 kuongeza fursa za ajira kwa vijana wetu.Tuongeze thamani ya uwekezaji, kuongeza ajira na kukuza uchumi. “











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad