Kaimu Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere John Baitani akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani
Na Khadija Kalili, Michuzi TV
SHULE ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere ya Kibaha Mkoani Pwani imeanza kutoa Mafunzo ya Uongozi, usimamizi wa fedha za serikali na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato kwa Viongozi wa Shule za Sekondari ikiwa ni katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji wa kazi zao za kila siku mashuleni.
Akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo ya siku tatu kutoka Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere ya Kibaha Mkoani Pwani John Baitani amesema Mafunzo hayo kwa Viongozi wa Shule pia watajifunza kuhusu Usalama wa nchi, Itifaki, uzalendo na Umajumui.
Mafunzo mengine ni pamoja na matumizi ya takwimu, jinsi ya kuongeza mapato bila kuvunja sheria, jinsi ya kuenenda Walimu wakiwa ni watendaji wa serikali ambayo ni kulingana na mapungufu waliyoyaona baina yao.
"Tuna wafundisha masuala mbalimbali kwakuwa wao ni Viongozi Wakuu wa Shule hasa ikizingatia wao ni Viongozi na wafanya maamuzi katika utendaji kazi wao wa kila siku" amesema Baitani.
Aidha Baitani amewataka Watanzania kuchangamkia matumizi ya miundo mbinu ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha ambayo inamilikiwa na nchi sita zilizoshiriki harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika hasa ikizingatia Shule hiyo imejengwa hapa nchini tofauti na ilivyo kwa zile nchi rafiki ambazo Shule imejengwa mbali na nchi zao.
Amesema Mafunzo hayo ni takwa la Uongozi wa umoja wa Waalimu Wakuu wa Shule unaofahamika kwa jina la TAHOSSA ambao walifika shuleni hapo kuomba Mafunzo hayo kwa Viongozi wa Shule za Wilaya ya Ilala ili kupata Mafunzo ya Uongozi kwa mujibu wa mitaala waliyokubaliana na Uongozi wa shule hiyo.
Mkurugenzi wa Taaluma Elimu ya Msingi Tanzania Alhaji Abdul Maulid amewataka walimu nchini kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro baina yao, wazazi na wanafunzi mashuleni sambamba na kufanya matumizi sahihi ya fedha zinazoletwa na serikali pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Amesema Walimu hao wamepatiwa mafunzo hayo ili kuwakumbusha maadili ya utendaji kazi wao kwenye mavazi na jinsi ya kuwalea watoto mashuleni uzalendo usalama wa nchi pamoja na mitaala mipya.
Aidha amewatahadharisha Waalimu hao kuwa Chama hicho cha Walimu Wakuu TAHOSSA siyo chama cha siasa hivyo wabaki kitaaluma zaidi na kuwasisitiza kujiandaa na kwenda kupiga kura kwa usalama na amani kwenye uchaguzi mkuu ujao na kuchagua viongozi bora katika ngazi ya Rais na Madiwani.
Aidha amegusia suala la waalimu kutoa adhabu kwa wananfunzi na kuwasisitiza waache kutembea na viboko kwa sababu ni kinyume na utaratibu pili Mwalimu anapokua anamuadhibu mwanafunzi ahakikishe hana ghadhabu zake kwani kumekuwa na taarifa nyingi za matokeo ya waalimu huleta madhara makubwa kwa wanafunzi pindi wanapokuwa wakiwapa adhabu (kuwachapa).
"Waalimu pindi mnapotoa adhabu kwa wanafunzi mnapaswa kuangalia afya ya mwanafunzi husika ili kukwepa kupata changamoto na ikibidi Mwalimu anapolazimika kutoa adhabu kwa mwanafunzi atumie adhabu mbadala na siyo viboko" amesema Maulid.
" Nendeni mkaifanye shule kuwa sehemu salama na tunapowaadhibu mwisho viboko ni vinne tu na hili limewekwa wazi mtoto wa kike anatakiwa aadhibiwe na nani na achapwe wapi kadhalika kwa mtoto wa kiume imeainishwa wapi achapwe na idadi ya viboko," amesema Maulid.
"Nendeni mkavumiliane , kazi yenu inahitaji kuwa na uvumilivu wa hali ya juu hivyo viongozi mkavumiliane Shule ni Taasisi ambayo inahitaji kuwa na mahusiano mazuri na jamii pia amewataka waalimu wakaziongoze shule kwa kusimamia miongozo iliyowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.
Katibu wa TAHOSSA Bi Sifa Mwaruko ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Viwege iliyopo Kata ya Majohe Wilayani Ilala amezungumza kwa niaba ya washiriki 70 amesema kwa niab…
[10:50 AM, 4/6/2025] Hadija Kalili: Kaimu Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere John Baitani akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani
No comments:
Post a Comment