jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

WATENDAJI WA UBORESHAJI TANGA, PWANI WATAKIWA KUFUATA SHERIA, KUHAMASISHA WANANCHI

Share This





Mjumbe wa Tuhe Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Asina Omari akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa Uboreshaji Mkoa wa Pwani. Mafunzo hayo yamefungwa leo Februari 03,2025 ambapo amewataka watendaji hao kutekeleza jukumu la kuhamasisha wananchi wa maeneo yao kushiriki kwenye uboreshaji kwa kushirikiana na wadau wengine wa uchaguzi.
MTM_9310
Mjumbe wa Tuhe Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magadalena Rwebangira akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa Uboreshaji Mkoa wa Tanga. Mafunzo hayo yamefungwa leo Februari 03,2025 ambapo amewataka watendaji hao kutekeleza jukumu la kuhamasisha wananchi wa maeneo yao kushiriki kwenye uboreshaji kwa kushirikiana na wadau wengine wa uchaguzi.
c80bf8c4-b364-41d2-b369-49125d33faee
Na Mwandishi wetu, Tanga na Pwani
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Mikoa ya Tanga na Pwani kuzingatia Katiba ya nchi, sheria za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na kanuni zake katika utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Asina Omari wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi na Maafisa TEHAMA Mkoani Pwani leo Februari 03,2025.

“Mnapaswa kutekeleza majukumu mliyopewa kwa kuzingatia Katiba ya nchi, sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na kanuni zilizotungwa chini ya vipengele vya sheria hiyo vinavyohusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,”alisema Mhe. Jaji Asina.

Aidha, alitoa wito kwa watendaji hao kuhakikisha kuwa wanaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia maelekezo yote waliyopewa ili kuongeza uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

“Ni matarajio ya Tume kuwa, mara baada ya zoezi hili kukamilika watu watakaokuwa wamepatiwa kadi watakuwa ni wapiga kura halali wa kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani” amesema Mhe. Jaji Asina.

Akifunga mafunzo kama hayo Mkoani Tanga nakuhusisha washiriki kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe, Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Magdalena Rwebangira amewataka watendaji hao kutekeleza jukumu la kuhamasisha wananchi wa maeneo yao kushiriki kwenye uboreshaji kwa kushirikiana na wadau wengine wa uchaguzi.

“Mnahimizwa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao,” alisema Mhe. Rwebangira.

Alisisitiza kuwa jukumu la uhamasishaji linawahusu moja kwa moja wao watendaji, kwa kushirikiana na wadau wengine katika maeneo yao kupitia nyenzo mlizo nazo.

“Mabango na vipeperushi mtakavyopewa na Tume mvisambaze mapema katika shehia zote zilizopo katika mikoa yote mitatu ya Unguja. Kazi yenu kubwa ni kusimamia na kuendesha shughuli zote za uboreshaji katika shehia zote” amesema Mhe. Magdalena.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa ya Tanga na Pwani umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 ambapo vituo vitafunguliwa Saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:00 jioni.
4385e028-25a3-4f73-9b04-f20cf6020961Meza Kuu ya Mafunzo kwa Mkoa wa Pwani ikiongoza na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) akifuatilia mafunzo hayo mkoani Pwani.

816e2292-f14c-438e-9093-253769b29402

7088ccd4-84db-450c-9a6d-e221acaffa51
Washiriki wa Mafunzo kutika Mkoa wa Pwani wakiwa katika ufungaji wa mafunzo.
MTM_9298Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akiwa katika ufungaji wa mafunzo hayo mkoani Tanga.

MTM_9289Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndg. Kailima R.K akizungumza jambo na washiriki mkoani Tanga.

INEC9652

INEC9641
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Tanga wakifuatilia hotuba ya ufungaji.
INEC9616
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Tanga wakifuatilia hotuba ya ufungaji.
INEC9603
Mwenyekiti wa Mafunzo kutoka Mkoa wa Tanga, Ndg. Mwanaidi Nondo akizungumza jambo kuhusiana na mafunzo hayo waliyopewa.
INEC9543

INEC9529
INEC9522Washiriki wakifanya mazoezi kwa vitendo kwa kuandikisha wapiga Kura wapya, kuboresha taarifa na kufuta waliopoteza sifa.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad