jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

Walimu 1500 wa Mkoa wa Singida wafikiwa na Kliniki ya Samia

Share This
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendegu akizungumza na viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mara baada ya kufungua Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto za Walimu katika Kliniki iliyofanyika Singida.

WhatsApp%20Image%202025-02-12%20at%2011.59.10%20PM
Walimu wakiwa katika Kliniki ya kutatua changamoto yao iliyoratibiwa na CWT kwa kushirikiana na Serikali.

WhatsApp%20Image%202025-02-13%20at%2012.00.18%20AMBaadhi ya walimu wakipata huduma katika dawati la maafisa Utumishi Ofisi ya Rais na Utawala Bora katika Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto za Walimu iliyofanyika Mkoa wa Singida



*Ni Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto za Walimu nchini.

Na Mwandishi Wetu Singida
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na Serikali imedhamiria kutatua changamoto za walimu nchi nzima.

Katika hatua  hiyo CWT pamoja na Taasisi za Serikali wameanza uratibu wa ziara katika mikoa 20 kwa ajili ya kukutana na walimu ikiwa ni Taasisi zinazohusika na walimu kuchukua changamoto zinazowakabili kwa ajili kufanyia kazi.

Madai ya walimu kuongezwa madaraja bila kupandishiwa mishahara,Malipo ya Likizo, Malipo ya uhamisho yote hayo.

Wakizungumza katika Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto za Walimu kwa Mkoa wa Singida walisema serikali ya awamu ya Sita inakwenda kumaliza changamoto zao.

Wamesema kuwa madai yao ya muda mrefu hivyo hawana shida na serikali kwa imani yao kuwa changamoto zinakwenda kutatuliwa.

Katika ziara ya kutatua changamoto za Walimu. kwa Mkoa wa Singida zaidi ya Walimu  1500 w wamefikiwa na Kliniki ya Samia ya Walimu ya kutatua changamoto zao.

Ziara ya kutatua changamoto za walimu inaratibiwa na Chama cha Walimu (CWT) kwa kushirikiana na Serikali katika kuwafikia Walimu kutoa changamoto za madai yao kwa ajili ya Serikali kufanyia kazi.

Akizungumza wakati akifungua Kliniki ya Walimu Mkoa Singida  Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendegu amesema kuwa Kliniki ya Samia ya Walimu inakwenda kutatua changamoto ya madai ya Walimu.

Amesema kuwa Kliniki ya Walimu kuanzishwa kwake ni matokeo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kutambua mchango wa Walimu hivyo wanahitaji kutatuliwa kwa kulipa madai yao.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa Walimu wa Mkoa wa Singida wamejitoa sana katika kufundisha licha ya kuwa na madai  na kufanya Mkoa kuendelea kufanya vizuri katika elimu.

 Afisa Utumishi Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Judith Abdallah  amesema wamejipanga katika kutatua changamoto za Walimu katika Kliniki ya  Samia na kuleta matokeo.

Amesema kuwa walimu  wamejipanga kutoa huduma kwa idadi iliyofika huku akidai madai mengine ni maelekezo.

Makamu  wa rais wa Chama cha Walimu (CWT) Seleman Ikomba emesema zoezi la kutatua changamoto za walimu ni endelevu .

Amesema kuwa Chama kimejipanga kushirikiana na serikali katika kufanya utatuzi wa madai ya walimu hivyo hawatakubali atokee mtu kuhujumu.

Aidha amesema katika kipindi hiki watashughulika na wahujumu ambao ni walimu katika kuweka utulivu huku serikali ikifanya mchakato wa ulipaji wa madai yao.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad