MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Usimamizi wa Masoko ya Fedha (CMSA),imetoa pongezi kubwa kwa Tanzania Commercial Bank kwa kuwa benki ya kwanza nchini kurahisisha upatikanaji wa hisa kwa njia ya TCB Popote Mobile App.
Akizungumza leo
Februari 21,2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya
Tanzania Commercial Bank (TCB) na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE),
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo ACPA. Nicodemus Mkama amepongeza
ushirikiano huo kwani ni hatua kubwa katika juhudi za kukuza ushiriki wa
wananchi kwenye masoko la mitaji na kuimarisha maendeleo ya sekta ya
fedha nchini.
“Hatua hii ni sehemu ya mapinduzi makubwa ya
kidijitali katika masoko ya mitaji na inakwenda sambamba na juhudi za
CMSA na DSE za kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa wananchi katika
uwekezaji wa soko la hisa.
“Umuhimu
wa ushirikiano huu kwa sekta ya Masoko ya mitaji ni moja ya nyenzo
muhimu ya kukuza uchumi wa taifa kwa kuwa yanatoa fursa kwa mashirika
na watu binafsi kuwekeza na kupata fedha za kukuza biashara zao.
Kupitia ushirikiano huu:
“Wananchi wengi zaidi watapata nafasi ya
kuwekeza Kupitia teknolojia ya simu ya mkononi, wananchi waliokuwa na
changamoto za upatikanaji wa huduma za soko la mitaji sasa wataweza
kushiriki kwa urahisi,”amesema.
Ameongeza ongezeko la mtaji kwa
makampuni yaliyoorodheshwa kuwa na njia rahisi ya kununua na kuuza hisa
kutachochea mahitaji ya hisa na kuongeza uhai wa soko la mitaji.
Pia
amesema ushiriki wa vijana na wajasiriamali katika uwekezaji teknolojia
hiyo inatoa fursa kwa vijana na wafanyabiashara wadogo kuanza safari
yao ya uwekezaji mapema kwa mtaji mdogo, hali inayoongeza ushirikiano wa
sekta binafsi na sekta ya kifedha.
Amefafanua mfumo huo wa
uwekezaji kupitia simu za mkononi utaongeza matumizi ya teknolojia na
kusaidia katika mkakati wa taifa wa uchumi wa kidijitali.

ACPA
Mkama amesema CMSA inahakikisha kuwa masoko ya mitaji nchini
yanaendeshwa kwa uwazi, usawa, na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa
vya usimamizi wa kifedha na kupitia mfumo huo wa kidijitali wawekezaji
watalindwa dhidi ya udanganyifu wa kifedha.
“TCB Popote Mobile
App imetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya usalama wa kifedha,
kuhakikisha kuwa uwekezaji wa wananchi unalindwa.Urahisi wa kupata
taarifa za soko la hisa kwa wakati halisiMwekezaji ataweza kufuatilia
bei za hisa, mwenendo wa soko, na maamuzi ya uwekezaji bila kutegemea
taarifa zisizo rasmi.
“Kuimarika
kwa uelewa wa wananchi kuhusu uwekezaji CMSA kwa kushirikiana na DSE na
taasisi za kifedha kama TCB, itaendelea kutoa elimu kwa umma ili
kuhakikisha wananchi wana uelewa sahihi kuhusu masoko ya mitaji.”
Ametoa
rai kwa wananchi wote kutumia fursa hiyo mpya ya kununua na kuuza hisa
kupitia TCB Popote Mobile App. Hiyo ni nafasi ya kipekee kwa kila
Mtanzania kushiriki katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa njia salama na
ya kidijitali.
Amesema Serikali kupitia CMSA itaendelea
kushirikiana na wadau wote wa sekta ya mitaji kuhakikisha kuwa masoko
yetu yanakuwa imara, yenye uwazi, na yanayowapa wananchi fursa za
kuwekeza kwa manufaa yao na kizazi kijacho
.jpeg)


No comments:
Post a Comment