jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

TIMU YA MATI SUPER BRANDS LTD YACHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA BENKI YA NMB

Share This
Na Ferdinand Shayo, Manyara.

Timu ya mpira wa miguu ya Wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited mkoani Manyara imecheza mechi ya kirafiki na timu ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Babati kwa lengo la kujenga umoja na ushirikiano wa kibiashara utakaoleta tija katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii mkoani hapa.

Nahodha wa Timu ya Mati Super Brands Limited ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo David Mulokozi amesema kuwa mechi hiyo ya kirafiki inalenga kuimarisha afya ya mwili ili kuongeza ufanisi mahali pa kazi.
InShot_20250126_134430037
Mulokozi amesema kuwa michezo kama hii inadumisha undugu,umoja na upendo sehemu za kazi na kuwataka wakuu wa Taasisi mbali mbali kujenga utamaduni wa kushiriki michezo pamoja na Wafanyakazi.

“Tumefanya mechi hii ya kirafiki kwasababu sisi Mati Super Brand Limited na Benki ya NMB ni marafiki lakini tunadumisha afya njema, hiki tulichokifanya leo naomba kiendelee” Anaeleza David Mulokozi Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited.
IMG-20250126-WA0015
Mdhibiti Ubora Benki ya NMB Tawi la Babati Donald Kipung`a amesema kuwa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd ni wadau wakubwa wa benki hiyo na kuahidi kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na kampuni hiyo inayoongozwa na Mkurugenzi wake David Mulokozi.
InShot_20250126_134925444
Amesema NMB kama wadau wa sekta ya fedha wataendelea kudumisha ushirikiano mzuri kati yao na taasisi binafsi ikiwemo Mati Super Brand Limited.
IMG-20250126-WA0027
IMG-20250126-WA0025
IMG-20250126-WA0023
Timu ya mpira wa miguu ya Wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited mkoani Manyara imecheza mechi ya kirafiki na timu ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Babati kwa lengo la kujenga umoja na ushirikiano wa kibiashara utakaoleta tija katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii mkoani hapa.
IMG-20250126-WA0034
IMG-20250126-WA0032
Mtanange ukiendelea...

Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad