jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

RAIS SAMIA-TUMELENGA KUONGEZA MEGAWATI 2,463 ZA NISHATI KUTOKANA NA VYANZO MCHANGANYIKO IFIKAPO 2030

Share This
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

RAIS wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema wamejipanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko ambapo mpaka sasa Tanzania inauwezo wa kuzalisha megawati 3,431 ambapo asilimia 58 inatokana na vyanzo vya maji, asilimia 35 ni gesi asilia na asilimia 7 inatokana na vyanzo vingine.

Ameyasema hayo leo Januari 28, 2025 wakati akihutubia mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa tumelenga kuongeza megawati 2,463 za nishati kutokana na jua, gesi asilia, upepo na vyanzo vingine ifikapo 2030.

Aidha Rais Samia amesema kuwa Tanzania ni kiungo muhimu katika kuunganisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na nishati ya umeme, jambo linalowezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Cairo, Misri.

"Tayari tumeshaunganisha miundombinu ya umeme na nchi za Burundi, Rwanda, Kenya na sasa tunaendelea kuunganisha umeme na nchi ya Zambia na Uganda ambapo uwepo wa miundombinu hii utawezesha biashara ya nishati kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC". Amesema

Pamoja na hayo amesema kuwa Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme, hadi mwezi Novemba 2024 mahitaji ya umeme nchini Tanzania yalikua megawati 1,888 wakati uzalishaji ni megawati 3,431.

"Tumepanga kufikisha umeme kwenye vitongoji vyote, baada ya kufanikiwa kusambaza umeme katika vijiji vyote vya Tanzania ambapo mwelekeo wetu wa sasa ni kuvifikia vitongoji vyote 64,359 ambapo mpaka sasa mpango wetu umeshavifikia vitongoji 32,827 na kazi inaendelea ya kuvifikia vitongoji vilivyobaki". Amesema

Amesema Tanzania ina Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya kupikia unaolenga kupandisha kiwango cha matumizi ya nishati safi ya kupikia kutoka asilimia 10 ya sasa hadi asilimia 80 ifikapo mwaka 2030, ambapo mpango mahususi tunaozindua leo utatusaidia kufikia lengo hilo.

40
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2025. 50,
61
66%20copy
MSN_0379
MSN_0433%202
MSN_0506
Matukio mbalimbali wakati wa mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2025.
28

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati tarehe 28 Januari, 2025. 35

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2025.36

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2025.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad