Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, amepokea kiasi cha shilingi milioni 10 kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kama pongezi kwa ushindi wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes). Timu hiyo ilishinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Timu ya Taifa ya Burkina Faso katika mchezo wa fainali wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika tarehe 13 Januari 2025, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Hundi hiyo ilikabidhiwa kwa Mhe. Rais na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Bi. Lulu Mengele, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba. Kulia kwa Mhe. Rais ni Mhe. Mama Mariam Mwinyi, na kushoto kwake ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Maulid Mwita, pamoja na Mhasibu wa NSSF, Bi. Sirinael Mwakyusa.
NSSF ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa Kombe la Mapinduzi 2025.
Post Top Ad
NSSF YAIPONGEZA ZANZIBAR HEROES KWA USHINDI WA KOMBE LA MAPINDUZI
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
Newer Article
Rais Samia ahutubia Mabalozi ,Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar
Older Article
Jumanne ya Ushindi Hii Hapa
NAFASI ZA UONGOZI WA SERIKALI ZA MASHEHA ZANZIBAR UNADAIWA KUTOZINGATIA USAWA WA KIJINSIA
Othman MichuziJan 19, 2025Kilimanjaro International Marathon 2025 yazinduliwa Moshi
Othman MichuziJan 18, 2025MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI MIKOA YA MTWARA, LINDI NA RUVUMA YAFUNGULIWA LEO
Ahmad MichuziJan 17, 2025
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment