Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla,
MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unatarajia kufanyika Januari
18 hadi 19 mwaka huu ukiwa na ajenda tatu ikiwemo kuziba nafasi ya
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.
Akizungumza na waandishi
wa habari Makao Makuu ya CCM katika ukumbi wa White House jijini Dodoma
leo, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla,
amesema mkutano mkuu huo utakuwa na ajenda tatu.
Alizitaja ajenda
hizo hizo ni kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara kufuatia
kujiuzulu kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Ndugu Abdulrahman
Kinana,kupokea kazi za Chama kuanzia mwaka 2022 hadi 2025 pamoja na
kupokea taarifa ya utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Ameeleza
kuwa taarifa hizo za utekelezaji ilani ni kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)
Kuhusu
mchakato wa kumrithi Kinana, amesema mrithi wa nafasi hiyo anatarajiwa
kupatikana baada ya kamati kuu kuwasilisha mapendekezo ya jina kwa
halmashauri kuu kisha halmashauri kuu kuwasilisha jina hilo kwa wajumbe
wa mkutano mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura.
"Kumekuwa na uvumi,
unaona vichwa vya habari kwamba CCM patashika, wafuatao watajwa kurithi
nafasi ya Kinana, nani kati ya hawa atachukua nafasi ya Kinana, wengine
wanakwenda mbali kuandika wafuatao kuchukua nafasi ya Kinana. Kila mmoja
anaandika navyotaka.
"Nataka kusema kwamba, nafasi ya Makamu
Mwenyekiti haigombewi, unaposema kinyang'anyiro kinatoka wapi wakati
nafasi haigombewi wala haijazwi fomu?," alieleza.
CPA Makala
alisisitiza: "Tutampata makamu mwenyekiti baada ya mapendekezo ya kamati
kuu na halmashauri kuu, kisha jina la atakayeziba nafasi hiyo
litawasilishwa katika mkutano kuu na hapo ndipo zitapigwa kura ya ndiyo
au hapana."
"Hatukuwa kimya, Chama kinaongozwa kwa katiba, kina
utaratibu wake, hatuwezi kuongozwa kwa hisia za watu. Kwa sasa Kamati
Kuu imeona ndiyo muda muafaka kujaza nafasi hiyo," alisema.
CPA
Makalla aibainisha kuwa mkutano mkuu utatanguliwa na vikao vya Kamati
Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, vinavyotarajiwa kufanyika Januari 16
mwaka huu.
Post Top Ad

MAKAMU MWENYEKITI TANZANIA BARA KUJULIKANA JANUARI 19.
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
Newer Article
Benki ya CRDB yaanza kutoa mikopo ya ada shule za msingi, sekondari
Older Article
DKT NCHEMBA AIPONGEZA TRA KUIMARISHA MAPATO
Benki ya Stanbic Tanzania yafuturisha wateja wake
Ahmad MichuziMar 21, 2025Ni miaka minne ya neema kwa Mashirika ya Umma
Othman MichuziMar 21, 2025Gawio kutoka kampuni ambazo Serikali ina hisa chache zapaa kwa asilimia 236
Othman MichuziMar 21, 2025
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment