Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam. Kampuni inayojulikana kwa ubunifu katika sekta ya michezo ya kubahatisha, M-Bet Tanzania, imezindua muonekano mpya wa tovuti yake kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja.
Tovuti hiyo, inayopatikana kupitia www.m-bet.co.tz, inawawezesha wateja kubashiri aina mbalimbali za michezo na kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha kwa urahisi zaidi. Kupitia tovuti hiyo pia unaweza kucheza Aviator na defender bila ya kwenda Casino.
Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Levis Paul, amesema kuwa uboreshaji huo ni hatua ya kuthamini wateja na kuwapa huduma bora zaidi ambapo ili kujiunga unajisajili kwenye tovuti hiyo www. m-bet.co.tz na kufuata maelelezo ambapo kwa wateja wa zamani, wanatakiwa kujiunga na kuingiza neno siri (password) upya.
"Mbali na kuwa na odds kubwa, tumeamua kuboresha tovuti yetu ili kuwarahisishia wateja wetu. Sasa wanaweza kucheza michezo kama aviator na defender bila kutembelea casino, kupitia simu ya mkononi, laptop, au kompyuta ya nyumbani," alisema Levis.
Kwa mujibu wa Levis, M-Bet imekuwa mstari wa mbele katika sekta ya michezo ya kubashiri nchini kwa zaidi ya muongo mmoja. "Tumekuwa sehemu ya ukuaji wa sekta hii, na mchango wa wateja wetu ni muhimu sana. Tunataka kuhakikisha wanapata thamani ya fedha zao na huduma zenye viwango vya juu," aliongeza.
Tovuti hiyo mpya inatoa nafasi kwa wateja kuweka mkeka, kushiriki au kubashiri katika michezo mbalimbali, na kuchukua ushindi wao papo hapo. Levis alibainisha kuwa maboresho haya ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kampuni hiyo kuhakikisha kuwa kila mteja anapata huduma bora zaidi.
Alisema kuwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 10, M-Bet imejijengea sifa kama waanzilishi wa michezo ya sports betting nchini Tanzania. "Tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya sekta hii, na tunawahakikishia wateja wetu kwamba tutaendelea kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji yao," alisema Levis.
Alifafanua kuwa wa maboresho haya, M-Bet Tanzania inadhihirisha dhamira yake ya kuwawezesha wateja kushiriki michezo ya kubahatisha kwa njia salama, rahisi, na ya haraka. Tovuti hii ni hatua kubwa katika kuwapa wateja huduma zinazolingana na mahitaji yao ya kila siku.
Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Levis Paul akizungumza wakati wa utambulisho mpya wa tovuti ya kampuni hiyo ambayo imeboreshwa na kuwa ya kisasa na kuwawezesha watejawao kubashiri
No comments:
Post a Comment