Msaidizi Ukaguzi na Uhiari wa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Maigloria Saria akizungumza na Wakurugenzi watendaji wa kampuni ya Uwakala wa Fedha GAF International Limited wakati walipomtembelea katika kituo chao cha kazi jijini Dar es Salaam leo Desemba 14,2024. Ikiwa ni kampeni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwatembelea Walipakodi kwaajili ya kuwashukuru kwa kuwa Walipakadi mzuri katika kipindi hiki cha Desemba.
Daktari wa B&B Polyclinic, Bhavin Jani akizungumza jijini Dar es Salaam leo Desemba 14,2024 na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walipofika katika kituo chake cha kazi kwaajili ya kumshukuru kwa kuwa mlipakodi mzuri. Wafanyakazi wa TRA wamefika hapo ikiwa ni kwaajili ya Kumshukuru, mkumsikiliza kero zake katika ukusanyaji wa Mapato katika kipindi hiki cha Desemba.
Msaidizi Ukaguzi na Uhiari wa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Maigloria Saria akimshukuru Daktari wa B&B Polyclinic, Bhavin Jani kulia wakati walipomtembelea katika kituo chake cha kazi jijini Dar es Salaam leo Desemba 14,2024. Ikiwa ni kampeni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwatembelea Walipakodi kwaajili ya kumshukuru katika kipindi hiki cha Desemba.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakurugenzi watendaji wa kampuni ya Uwakala wa Fedha ya GAF International Limited wakati walipomtembelea katika kituo chao cha kazi katikaeneo la Goba jijini Dar es Salaam leo Desemba 14,2024. Ikiwa ni kampeni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwatembelea Walipakodi kwaajili ya kuwashukuru kwa kuwa Walipakadi mzuri katika kipindi hiki cha Desemba.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Tegeta katika eneo la Goba Centre jijini Dar es Salaam walipoweka kambi kwajili ya kuwasogezea karibu huduma walipakodi katika kipindi hiki cha Desemba. Ikiwa ni kampeni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwatembelea Walipakodi kwaajili ya kuwashukuru kwa kuwa na kuwasogezea huduma karibu walipakodi.
WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Kikodi wa Tegeta katika eneo la Goba wameishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwatambua kuwa ni walipa kodi wazuri.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Desemba 14, 2024 alipotembelewa na uongozi wa TRA katika eneo lake la kazi Dkt, Bhavin Jani wa B&B Specialized Polyclinic amesema TRA wamethamini Mchango ambao wanautoa kama kituo na kwa kulipakodi Vizuri.
"Tunashukuru sana kwa kuthaminiwa lakini bado tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kwamba nchi yetu kwa pamoja tunasonga mbele na kuhakikisha maendeleo yanapatikana nchini." Amesema Dkt. Jani
Pia amewapongeza kitengo cha huduma kwa wateja cha TRA.... "Kimeboreka sana katika kipindi hiki cha 2024."
Pia amewapongeza kwa kuendelea kuboresha mifumo mbalimbali ya kodi licha ya kuwa bado wanapata changamoto chache kama ukilipa kodi lakini mfumo usitambue kama umelipa kodi.
Tunaamini katika mazungumzo yetu wataenda kufanyia kazi changamoto hiyo kwahiyo kwa 2025 pengine kutakuwa na mabadiliko zaidi katika kulipa kodi.
Akizungumza na TRA walipofika Ofisi za kampuni Uwakala wa Fedha, Mkurugenzi wa GAF International Group Limited, Flora Erasto amewashuru TRA Kwa kutambua kuwa wao ni walipa kodi wazuri... "Sisi hilo tunaliamini kwani tumekuwa tukilipa kodi vizuri tunashukuru kwa kutupa huo umhimu na hiyo nafasi ya kuja kutushukuru huduma tunayoipata ni nzuri kwa kweli." Amesema Flora.
Amesema endapo wakipatwa na changamoto yeyote wamekuwa wakifika kwa viongozi ambao wanahusika na faili lao na kama kunachangamoto yeyote imekuwa ikitatuliwa na wao wamekuwa wakilidhika na utatuzi wa changamoto hizo.
Pia wameahidi kuwa wataendelea kuitambua TRA na kuweza kufanya yale yote ambayo wanatakiwa kufanya katika biashara zao."
Kwa upande wake, Msaidizi Ukaguzi na uhiari wa Ulipaji wa Kodi, Maigloria Saria, baada kuwatembelea Walipakodi wa Goba, amesema kuwa TRA katika kampeni yake ya mwezi huu wa Desemba wameanza kuwatembelea walipakodi nchini kwa ajili ya kuwashukuru na kuwasikiliza na kuwasogezia huduma karibu.
Amesema katika kudumisha mwezi huu wa Desemba wamepita katika biashara za walipakodi wa Mkoa wa Kikodi Tegeta katika eneo la Goba kwa ajili ya kuwasikiliza na kuchukua maoni yao katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Pia amesema wamesikiliza kero zao na changamoto zao ili kuwawezesha kulipa kodi zao bila usumbufu.
Katika kusogeza huduma karibu wameweka hema katika eneo la Goba Centre ili wateja wafike kupata huduma mbalimbali zinazotolewa katika Ofisi za TRA.
Maigloria amesema lengo ni kumaliza mwezi huu wa Desemba na watu kwenda kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka wakiwa wamelipa kodi zao kwa wakati ili kuchangia katika maendeleo ya nchi.
Aidha Ametoa rai kwa walipakodi hususani wa eneo la Goba kutumia hema lililowekwa katika eneo la Goba centre kwa ajili ya kujipatia huduma hata zile ambazo hutolewa ofisini ikiwa pamoja na kulipa kodi kwa hiari.
Hema hilo litakuwepo katika eneo la Goba centre kuanzia leo Desemba 14 hadi Desemba 31, 2024.
"Hivyo tuwasisitize na kuwasihi mfike kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na TRA na kuweza kulipa kodi kwa wakati pale mnapomaliza mwaka mkiwa hamna madeni na kuuaza mwaka mpya vyema.
No comments:
Post a Comment