MWENYEKITI wa Tume ya Haki za Binadamu na Tawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema haki za binadamu Tanzania bado tupo vizuri kuliko nchi yeyote duniani.
Hayo ameyabainisha leo Desemba,14 2024 jijini Dar es Salaam, Jaji Mwaimu wakati wa Wanafanya maadhimisho ya haki za binadamu duaniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Desemba, 10 na yenye Kauli mbiu ya; Haki zetu, maisha yetu, sasa na baadae.
Amesema hakuna nchi duniani inaweza kusema kwamba inazingatia haki za binadamu kwa asilimia 100 ili wanazidiana kwa viwango.
"Tanzania hatuko vibaya tupo vizuri pamoja na changamoto ambazo tunazo bado Tanzania tutafanya vizuri, kwa mfano maeneo ya habari kuna malalamiko ndio watu hawapati fursa ya habari pengine maafisa wanapokwenda katika ofisi unakuta hawapo hawapati taarifa stahiki lakini serikali imetoa maelekezo kila wizara au taasisi lazima iwe na wasemaji kwa sasa Serikali iliweka utaratibu huu," amesema Jaji Mwaimu.
Amesema huwa wanaadhimisha haki za binadamu duniani yanatokana na tamko la dunia kuhusu haki za binadamu lilotolewa mwaka 1948 lililenga katika kuratibisha haki mbalimbali za binadamu.
Amesema Lengo la maadhimisho haya ni Kutafakari kwa pamoja kauli mbiu ya mwaka huu kwa kushirikiana na wadau na wageni mbalimbali waliohudhuria.
Ameeleza kuwa wataendelea kuhamasisha haki za binadamu na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi watajadili kuwa kila binadamu anahaki za msingi na haki za binadamu hazi gawanyiki ila zinategemeana.
Ameongeza kuwa kuimarisha mifumo ya utoaji haki na kulinda haki za makundi maalum watoto, walemavu na wengineo na wote wanakumbusha kulinda haki zao.
Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Tawala Bora, Patiance Mtwina amesema kila mwaka huadhimisha siku ya haki za binadamu kwa kusikiliza hoja mbalimbali, kutatua changamoto na kupokea malalamiko ya wananchi ili kuweza kuwasaidia.
"Tumekuwa kwa siku tatu katika Wilaya ya Temeke kwaajili ya wananchi wa Temeke ambapo tulipokea shida za migogoro ya ardhi tunafanyia kazi wananchi wengi wana migogoro ya ardhi," amesema.
Ametaja baadhi malalamiko waliopokea ni pamoja na mirathi imekuwa tatizo kwa wananchi, faida za bima wanapopata ajali, mafao na wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kuifikia Tume hiyo.
Kwa upande wake, Mwanasheri wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Richard Shumbusho, amesema ni muhimu haki za binadamu nchini zilindwe haki si ya mtu mmoja ni jamii nzima.
No comments:
Post a Comment