Kampuni ya usambazaji na uuzaji wa huduma na bidhaa za nishati ya Puma Energy Tanzania imetwaa tuzo ya Kituo Bora cha Mafuta kinachofikika na kupatikana kwa urahisi zaidi Tanzania katika tuzo za Consumer Choice Awards Africa (CCAA) 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa The Super Dome – Masaki, jijini Dar es Salaam.
Kampuni
hii inajivunia mtandao wake mpana wa vituo vya utoaji wa huduma na
bidhaa za nishati kwa teknolojia ya kisasa na huduma kwa wateja ya hali
ya juu. Mteja anapotembelea vituo vyake hupata zaidi ya huduma ya
ujazaji wa mafuta kwasababu anaweza kufanya manunuzi ya mitungi ya Puma
Gas, mahitaji mbalimbali ya nyumbani kupitia duka lililopo, ukaguzi wa
gari, huduma ya uoshaji, ujazaji upepo matairi, pamoja na bidhaa bora za
vilainishi ili kumfanya asikwame katika safari yake.
Kupitia
uwekezaji wa upanuzi wa vituo vipya ili kuwafikia wateja na Watanzania
nchini kote, Puma Energy Tanzania huhakikisha inawezesha jamii
inapoendeshea shughuli na kutoa huduma zake. Kampuni huzingatia kutoa
kipaumbele cha ajira kwa wakazi wa eneo husika ili kupunguza changamoto
ya ajira na kuiwezesha jamii kuchangia katika shughuli za maendeleo ya
kijamii na kiuchumi.
Katika tuzo hizo, Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo
alikuwa mgeni rasmi.
Tuzo
hiyo ya Kituo Bora cha Mafuta Kinachofikika na Kupatikana kwa Urahisi
Zaidi nchini, ilipokelewa na Mkurungenzi Mtendaji wa Puma Energy
Tanzania, Bi. Fatma M. Abdallah akiambatana na wafanyakazi kutoka idara
mbalimbali za kampuni hiyo.
Consumer
Choice Awards Africa (CCAA) ni tukio la kila mwaka la utoaji tuzo
ambalo linalenga kutoa tuzo kwa makampuni, mashirika na taasisi katika
barani Afrika katika sekta mbalimbali za uchumi kupitia maoni ya umma au
wateja yanayokusanywa kwa mtindo wa kura za mtandaoni kupitia tovuti ya
waandaaji. Tuzo hizi zilianzishwa mwaka 2019 jijini Dar es Salaam
Tanzania lakini pia hufanyika katika nchi zingine kama vile Kenya,
Malawi, na Afrika ya Kusini.
Tuzo
za mwaka huu wa 2024 zilifanyika wiki iliyopita, tarehe 30 Novemba
katika ukumbi wa The Super Dome Masaki, jijini Dar-es-salaam, Tanzania,
na kuhudhuriwa na makampuni 500 zaidi ya na wafanyabiashara kutoka
sehemu mbalimbali Afrika walishiriki, pia wageni mashuhuri kama vile
viongozi wakuu wa serikali walihudhuria.
No comments:
Post a Comment