jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

MILLIONI 200 ZA RAIS SAMIA ZALETA MAPINDUZI YA MIUNDOMBINU YA UTALII TABORA ZOO

Share This

WhatsApp%20Image%202024-12-13%20at%207.59.13%20AM
WhatsApp%20Image%202024-12-13%20at%207.59.15%20AM

WhatsApp%20Image%202024-12-13%20at%207.59.12%20AM

WhatsApp%20Image%202024-12-13%20at%207.59.11%20AM%20(1)

WhatsApp%20Image%202024-12-13%20at%207.59.11%20AM
* Mapato na Idadi ya watalii vyaongezeka

Na Mwandishi wetu, Tabora.
Zaidi ya TZS Millioni 220 zilizotolewa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya utalii ndani ya bustani ya wanyamapori hai "Tabora ZOO" zimekuwa chachu ya kuchechemua utalii wa ndani Mkoani Tabora.

Hayo yamesemwa Desemba 12, 2024 na Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Kanda ya Magharibi ya TAWA Jovin Nachihangu wakati akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ndani ya bustani hiyo ya wanyamapori hai.

"Kabla ya maboresho ya miundombinu ya utalii TAWA tulikuwa tunakusanya TZS Millioni 1 Kwa Mwaka, lakini baada ya maboresho katika kipindi hiki cha miaka 3 TAWA inakusanya kupitia bustani hii kiasi kisichopungua TZS Millioni 50 Kwa Mwaka na bado tunaendelea kuhakikisha kwamba mapato yanaendelea kuongezeka" amesema Jovin.

Aidha Jovin amebainisha miundombinu iliyoboreshwa ndani ya bustani hiyo kuwa ni jengo la wananchi kupata taarifa za vivutio vya utalii vinavyopatikana katika bustani hiyo na Kanda ya Magharibi Kwa ujumla (Visitors Information Centre - VIC), vyoo vya kisasa Kwa ajili ya wageni na mabanda ya wanyamapori walao nyama (Simba, Chui, Duma n.k).

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuiwezesha Taasisi ya TAWA kupata fedha za kuboresha miundombinu ya utalii katika bustani hiyo, jambo ambalo amesisitiza kuwa limekuwa chachu ya kuchechemua utalii wa ndani katika Mkoa wa Tabora

Maganja amesema katika kipindi cha miaka mitatu kabla ya maboresho walikuwa wakipata wageni wachache katika bustani hiyo

Amesema katika kipindi cha Mwaka 2021/22 bustani hiyo ilipokea wageni 308, na Kadri maboresho yalivyozidi kufanyika Taasisi hiyo ilishuhudia ongezeko la wageni ambapo Mwaka 2022/23 walipokea wageni zaidi ya 6,300 na katika kipindi cha Mwaka 2023/24 wameweza kupokea zaidi ya wageni 10,700 Jambo ambalo linaleta matumaini makubwa.

Naye Diwani wa Kata ya Kitete Mhe. Mussa Kayolo amesema Tabora ZOO imekuwa ni kivutio kikubwa Kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora kutokana na upekee wake wa kuwa katikati ya Manispaa ya Tabora, uwezo wa kufikika Kwa urahisi na wingi wa rasilimali wanyamapori na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo bustanini humo.

Mhe. Kayolo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha na kuwahamasisha wawekezaji wote wenye kiu ya kuwekeza, wawekeze katika bustani hiyo.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad