jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

Mawakala wa Forodha Sirari watakiwa kuzingatia sheria-Meja Gowele

Share This
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele  akizungumza na Mawakala wa Forodha wa Sirari mpaka wa Tanzania na Kenya katika Mkutano ulioandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
WhatsApp%20Image%202024-12-15%20at%205.17.32%20PM
Mtakwimu Mwandamizi  wa TASAC ,Athuman Athuman akizungumza kuhusiana na matakwa ya Sheria ya Uwakala wa Forodha kwa mawakala wa Forodha Sirari mpaka  wa Tanzania na Kenya.
WhatsApp%20Image%202024-12-15%20at%205.23.17%20PM
Mrakibu Mwandamizi wa  Idara ya Uhamiaji Daodatus Sonda akizungumza kuhusiana  kazi ya mawakala wa forodha katika mipaka.
WhatsApp%20Image%202024-12-15%20at%205.23.18%20PM
Mkurugenzi Mtendaji  wa Kampuni ya Uwakala wa Forodha ya Emaus Logistics Tanzania Limited Maryam Muhambo akizungumza kuhusiana kupewa elimu  kuhusiana na baadhi ya mawakala kutojua mipaka ya kazi yao.
WhatsApp%20Image%202024-12-15%20at%205.26.23%20PM
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele akisalimiana na Mtakwimu Mwandamizi  wa TASAC  kabla kikao kati ya wadau wa Uwakala wa Forodha katika mpaka wa Sirari,Tarime mkoani Mara.
WhatsApp%20Image%202024-12-15%20at%205.29.11%20PM
Baadhi ya mawakala wa forodha wakisikiliza wasilisho kutoka TASAC kuhusiana na sheria ya iliyoanzishwa kuhusiana mawakala wa Forodha.
WhatsApp%20Image%202024-12-15%20at%205.31.59%20PM
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele  akipata maelezo kutoka TASAC kabla ya kuanza kwa mkutano kwa Mawakala wa Forodha katika Mpaka wa Sirari.
WhatsApp%20Image%202024-12-15%20at%205.34.03%20PM
 Picha ya pamoja Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele pamoja na Taasisi za Serikali zinazofanya katika mpaka wa Sirari ,Mawakala wa Forodha.

*TASAC yaweka mikakati ya kutoa elimu kwa mawakala wa Forodha
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Sirari, Msoma.
MKUU wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele amewataka mawakala wa Forodha katika Mpaka Sirari kuzingatia sheria katika kufanya kazi mpakani hapo.

Meja Gowele ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa Mawakala wa Forodha uliondaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC uliofanyika katika Ofisi za TRA Sirari wilayani Tarime mkoani Mara.

Amesema kuwa Sheria zipo ambazo zinaongoza kazi ya Uwakala wa forodha hivyo lazima zifuatwe katika kuendelea nchi kupata mapato kwa ajili ya maendeleo mbalimbali.

Meja Gowele amesema kuwa mawakala wa Forodha wanatakiwa kuwa na ofisi ambazo zitasaidia TASAC kuwafikia na wakati changamoto zinapotokea kufanya urahisi wa kuzitatua.

Amesema kuwa kutokana na changamoto zinazojitokeza kwa kuwa na mawakala ambao hawajasajiliwa amewataka kuwa na vitambulisho ambavyo watatumia katika kufanya kazi katika eneo la mpaka wa Sirari kati ya Tanzania na Kenya.

Hata hivyo amesema katika mpaka huo kuna watu wanafanya uwakala wa forodha hawajasajiliwa na kufanya kuharibu taswira kwa watu waliopo kisheria ambapo mapato yao yanapotea kutokana na kuwa na hao mawakala wasiosajiliwa.

Mtakwimu Mwandamizi wa TASAC Athman Athman amesema kuwa mawakala wa forodha sheria ziko wazi katika kufanya kazi hiyo na wasipofuata sheria hatua zinachukuliwa.

Amesema kuwa katika kuhakikisha mawakala wanaotoa huduma za forodha TASAC kazi yake kutoa elimu katika kuwa na mawasiliano ambayo yanaboresha kazi zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uwakala wa Forodha ya Emaus Logistics Tanzania Limited Maryam Muhambo amesema changamoto zinatokana katika Mawakala wa Forodha ni elimu na kuiomba TASAC kufanya kikao na Viongozi Chama Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFF) ambao watakwenda kutoa elimu kwa wananchama wao.

Maryam amesema kuwa misingi ya kufanya kazi za uwakala wa forodha hivyo kazi ya mawakala ni kufuata ili kuepusha migongano na Taasisi za Serikali zinazodhibiti kazi hiyo.

Nae Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji katika Mpaka wa Sirari Deodatus Sanda amesema kuwa mawakala wataofanya udanganyifu watachukuliwa hatua.

Amesema ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Kenya uendelee kwa watu kutembea kilomita 10 kwa kila nchi na nje hapo hatua zitachukuliwa.

Amesema kwa madereva wanaoingia na magari biashara wanatakiwa kulipa na sio kutumia ujirani mwema wa kutembea kwa miguu.

Kaimu Meneja wa Forodha wa TRA Abdallah Salum amesema kuwa kazi wanaendelea kushirikiana na mawakala wa Forodha kufuata taratibu za kulinda mawakala wa Forodha kwa kutoruhusu watu wengine wasiokuwa na utalaam kufanya kazi hiyo.

Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad