NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho katika uchaguzi ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam, Lissu amesema kupitia nyazifa mbalimbali alizopitia ameshaona maeneo ambayo yanahitajika kutekebishwa akipata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho.
Amesema ameandika barua kwa Katibu Mkuu, kuondoa kusudio la kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, na amewasilisha barua ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa.
“Wanachama wenzangu wa CHADEMA, Katika uongozi wangu kwenye nyazifa mbalimbali kwenye chama ninaamini nanyi wanachama mnaamini yakuwa ninasifa za kutosha kabisa ya kugombea nafasi ya juu kabisa na kuweza kuongoza vizuri kupitia chama hiki”. Amesema
Amesema Mwanachama wa CHADEMA au Mtu mwingine anayeona ajabu au anachukizwa au kukwazwa na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho, atakuwa hajui au hataki kuenzi urithi walioachiwa na Wazee wao, Edwin Mtei na Bob Makani, kuachiana madaraka ya Uongozi ndani ya Chama kwa njia ya Uchaguzi huru na wa haki.
Aidha Lissu amesema Chama kinahitaji mawazo mapya kupitia uongozi mpya ili Chama kiweze kukua na kutekeleza yale ambayo yanahitajika.
Post Top Ad
LISSU ATANGAZA RASMI KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA
Share This
Tags
# SIASA
Share This
Jiachie Blog
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
Newer Article
KUTANA NA MAHARAMIA WA BAHARINI| BARBARY COAST KASINO
Older Article
TANDIKA JAMVI LAKO NA MERIDIANBET LEO
LISSU ATANGAZA RASMI KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA
Ahmad MichuziDec 12, 2024RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI
Ahmad MichuziNov 15, 2024CCM YATOA OMBI TAMISEMI WENYE MAKOSA MADOGO MADOGO KATIKA UJAZAJI FOMU UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAACHWE WAGOMBEE
Ahmad MichuziNov 12, 2024
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment