jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

JAY MELODY APAMBA UZINDUZI KIBAHA SHOPPING MALL

Share This

 

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akizungumza kwenye uzinduzi wa soko la kisasa litakalofahamika Kibaha Shopping Mall lililopo katikati ya kitovu cha Mji wa Kibaha karibu na Stendi ya mabasi yaendayo Mikoani barabara ya Morogoro Uzinduzi umefanyika leo tarehe 7 ,Desemba 2024.
WhatsApp%20Image%202024-12-07%20at%209.52.18%20PM
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba mwenye sauti  (katikati)akizungumza  kwenye uzinduzi  huo  na kuwasisitiza  wananchi wa Kibaha kutokwenda Dar  kwa sababu  wamezogezewa huduma muhimu kwenye soko hilo la kisasa Kibaha Shopping Mall
WhatsApp%20Image%202024-12-07%20at%209.54.56%20PM
Msanii Jay Melody  akiwa kwenye Jukwaa  na kusindikiza kwa burudani  kwenye uzinduzi  huo
WhatsApp%20Image%202024-12-07%20at%2010.02.29%20PM


Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji ametoa onyo kali kwa wapangaji wa maduka ambao wamepanga kwa lengo la kuwa madalali kuwa watachukuliwa hatua stahiki kutokana na kwenda kinyume na maombi yao ya kuwa wapangaji.

"Natoa onyo kwa wapangaji ambao wameomba na kupatiwa nafasi kwenye soko letu jipya na la kisasa Kibaha Shopping Mall kwamba tutafuatilia aliye panga ndiye anayetakiwa kufanya biashara na siyo kinyume cha hapo, hakuna udalali kwenye maduka yetu kama mtu akibainika anakuwa dalali tutamshughulikia mara moja pindi itakapo bainika" amesema Mkurugenzi Shemwelekwa.

Shemwelekwa amesema kuwa kwa kupitia soko hilo la kisasa wanatarajia kukuza ukusanyaji wa mapato ya ndani ,huku yatasaidia kwenye kununua madawa ,madawati , kujenga shule, zahanati na barabara ndani ya Kibaha.

Soko hilo la kisasa limezinduliwa leo tarehe 7 Desemba, 2024 na Mkuu wa Wilaya Kibaha Nickson Simon ambaye alikuwa mgeni rasmi.

"Leo ni siku ya burudani na biashara kwa wakaazi wa Kibaha na viunga vilivyopo jirani pia ikumbukwe kuwa safari ya ujenzi wa soko hili ilianza mwaka 2018 na kukamilika sasa hivyo nampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupa fedha , Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mwajuma Nyamka,Mbunge Silvestry Koka Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kibaha wote hawa wamechangia kufanikisha safari hii.

"Kuna fedha kidogo zimebaki tutajenga soko la wajasiriamali wadogo pembeni na tutawawekea mazingira rafiki ya biashara.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt. Rogers Jacob Shemwelekwa amesema kuwa ndani ya miaka mitatu ijayo mapato ya ndani yatakua maradufu kwa sababu wanategemea kukusanya zaidi ya Bil.15 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Kibaha.

"Kutokana na fedha za mapato yetu ya ndani tumeweza kuchonga barabara ,kujenga shule ya mchepuo wa Kiingereza na tumenunua eneo la maegesho Misugusugu" amesema Dkt.Shemwelekwa.


"Ujenzi wa soko hili umegharimu kiasi cha Bil.8 fedha ambazo zimetoka serikali kuu" amesema Shemwelekwa.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa huduma zinazopatikana ndani ya soko hilo kuwa wamo wafanyabiashara wenye nembo zote kubwa,huduma za benki, kuna sehemu imetengwa kwa ajili ya michezo ya watoto,sehemu za kuuza vyakula na vinywaji mbalimbali (bar).

"Huu ni mradi wa kimkakati pia matarajio yetu ni kukusanya kiasi cha Mil.660 kwa mwaka" anesema Dkt.Shemwelekwa.

Msanii Jay Melody amepamba uzinduzi huo pamoja na msanii mzwa wa Kibaha Smata.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad