Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA Ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA,) imezindua rasmi jukwaa la uwekezaji la M-WEKEZA ambao ni mradi wa pamoja wa kampuni ya Sanlam Investments East Africa Limited na M-PESA Limited na kuelezwa kuwa hiyo ni hatua muhimu katika maendeleo ya sekta ya fedha hususani masoko ya mitaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumza leo Novemba 21,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo Mkurugenzi Mkuu wa CSMA CPA. Nicodemus Mkama amesema uzinduzi wa jukwaa hilo utaimarisha na kuongeza kasi ya malengo ya kuwawezesha kifedha wafanyabiashara binafsi katika ukanda wa Afrika na kupitia M-WEKEZA jukwaa la uwekezaji kwa njia ya simu litawawezesha watu binafsi kupata fursa ya uwekezaji kwa urahisi katika maeneo ya mijini na vijijini kwa kutoa huduma za kifedha.
CPA Mkama amesema mpango huo unatoa fursa za uwekezaji kwa wawekezaji wakiwemo wanawake na vijana hali itakayochagiza maendeleo kwa kuhamasisha akiba ya ndani kupitia uwekezaji, kutengeneza fursa za ajira na kujenga uchumi thabiti wa Taifa.
“Uzinduzi wa jukwaa hili pia unaendana na mfumo wa tatu wa kitaifa wa ujumuishaji wa kifedha wa 2023/2028 ambao unasisitiza matumizi ya kidigitali katika usambazaji na utoaji huduma za kifedha.” Amesema.
Ameipongeza menejimenti ya Sansalam Investment East Africa Limited na M-PESA Limited kwa jitihada za kuunganisha mifumo yao na kupata kibali cha CMSA ambayo imeendelea kuweka mazingira rafiki ya kisera, udhibiti na utendaji yanayochagizwa na uimara wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
"Kazi kubwa ya masoko ya mitaji ni kukusanya rasilimali kutoka kwa wawekezaji na kuzielekeza kwenye uwekezaji wenye tija na kuchochea maendeleo katika Serikali, mamlaka za mitaa, taasisi kubwa na ndogo na kampuni mbalimbali ambazo hutoa fedha zinazoelekezwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo,"amesema CPA Mkama.
Post Top Ad
MAMLAKA YA MASOKO YA MITAJI NA DHAMANA YAZINDUA JUKWAA LA M-WEKEZA
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
Newer Article
Benki ya CRDB Yatoa Madawati 80, Viti na Meza 50 Wilayani Babati Mkoani Manyara
Older Article
NSSF YAWATAKA WATANZANIA KUJIWEKEA AKIBA
Serikali yaweka mikakati ya suluhu ya wezi katika mitandao
Othman MichuziNov 22, 2024WAFANYABIASHARA MSITUKIMBIE TUNAPOPITA KWENYE BIASHARA ZENU- TRA
Othman MichuziNov 22, 2024CHUO CHA VETA MKINGA KUTOA BURE HUDUMA YA UFUNDI UMEME KWA KAYA 50 WILAYANI MKINGA
Othman MichuziNov 22, 2024
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment