Timu
ya mpira wa kikapu ya wanawake, Fox Divaz kutoka Mara, imetwaa ubingwa
wa Tanzania betPawa NBL, baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya BD Lioness
ya Dar es Salaam.
Katika mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya
Chinangali jijini Dodoma, Fox Divaz waliibuka na ushindi wa pointi 67-54
dhidi ya BD Lioness na kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza.
Kwa
kutwaa taji hilo, Fox Divaz walikabidhiwa kombe na zawadi ya pesa
taslimu Shilingi milioni 2.8 kutoka kwa wadhamini wakuu wa mashindano
hayo, betPawa.
BD Lioness, waliomaliza nafasi ya pili, walipatiwa Shilingi milioni 2.4.
Katika
mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, Orkeeswa walipata ushindi wa mezani
kwa pointi 20-0 baada ya Viipers Queens kushindwa kufika uwanjani.
Orkeeswa walizawadiwa Shilingi 700,000.Zawadi zote zilikabidhiwa na
Nassoro Mungaya, Mratibu wa Masoko wa Kanda ya Afrika Mashariki wa
betPawa.
Mungaya aliwapongeza wachezaji wa timu zote, maofisa, na
wadau wa mpira wa kikapu kwa kujitokeza kwenye Uwanja wa Chinangali
kushuhudia mechi hiyo.
Alisema betPawa inajivunia kuwa mdau wa mchezo huo na kuahidi kuendeleza juhudi za kukuza hapa nchini.
"Tumejidhatiti
kukuza mchezo wa mpira wa kikapu nchini. Tumevutiwa na viwango vya
wachezaji, na naipongeza timu mshindi na zingine kwa kiwango kizuri
walichoonyesha katika mashindano yote huko Dodoma," alisema Mungaya.
Kwa
upande wake, kocha mkuu wa Fox Divaz, Bariki Kilimba, alisema kuwa
bidii na ari ya wachezaji wake ndiyo iliyowafanya kufanikisha ushindi
huo.
Kilimba alieleza kuwa kila mchezo ulikuwa mgumu, lakini
wachezaji wake waliweza kucheza kwa uwezo wao wa juu, jambo ambalo
limewafanya wakazi wa mkoa wa Mara kujivunia.
"Wachezaji wangu
wanastahili pongezi kwa ushindi huu. Walipambana sana ili kufanikisha
mafanikio haya. Tumeonyesha kuwa hata vilabu vya mikoani vinaweza
kuibuka na changamoto katika mchezo huu," alisema Kilimba.
"Tulicheza
jumla ya mechi tisa na kushinda nane. Hili ni rekodi, na wachezaji
wangu 12 pamoja na maofisa wanne walipokea Shilingi 1,260,000 kila mmoja
kama Locker Room Bonus kutoka betPawa. Tumehamasika kwa zawadi hiyo,"
aliongeza Kilimba.
Alisema malengo yao yanayofuata ni kufuzu kwa
mashindano ya Kanda ya Tano kwa mara ya pili mfululizo, kufuatia
mafanikio yao ya mwaka jana.
Mratibu
wa masoko wa Kanda ua Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Nassoro
Mungaya akikabidhi kombe kwa washindi wa mashindano ya betPawa NBL kwa
wanaume, timu ya Dar City ya mkoa wa Dar es Salaam.
Mratibu
wa masoko wa Kanda ua Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Nassoro
Mungaya akikabidhi kombe kwa washindi wa mashindano ya betPawa NBL kwa
wanawake, timu ya Fox Divaz ya mkoa wa Mara.
Mratibu
wa masoko wa Kanda ua Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Nassoro
Mungaya akikabidhi mfano wa hundi kwa washindi wa mashindano ya betPawa
NBL kwa wanawake, timu ya Fox Divaz ya mkoa wa Mara.
Mratibu
wa masoko wa Kanda ua Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Nassoro
Mungaya akikabidhi mfano wa hundi washindi wa mashindano ya betPawa NBL
kwa wanaume, timu ya Dar City ya mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment