Na Said Mwishehe, Michuzi TV
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiomba Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI) kupuuza dosari ndogondogo ambazo zimejitokeza katika ujazaji fomu kwa wagombea wa vyama vya siasa wanaoshiriki uchaguzi Serikali za mitaa nchini.
Sababu za kutoa ombi hilo kwa TAMISEMI imetokana na kuwepo kwa mapingamizi mbalimbali yaliyotokana na makosa ya kisheria katika ujazaji fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari leo Novemba 12,2024 katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk.Emmanuel Nchimbi amesema kuna mapingamizi kwa vyama vyote yanayotokana na kukiukwa kwa Sheria katika kujaza fomu hizo.
"Kwa sasa mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa uko katika kupitia rufaaa zilizotokana na mapingamizi yaliyosababishwa na makosa katika kujaza fomu, wapo waliokosea kuandika herufi za majina . Wengine katika nafasi inayotoka mgombea awe mwanamke lakini unakuta amejaza mwaname lakini wapo waliokosea kujaza tarehe ya kuzaliwa,"amesema.
Balozi Nchimbi amesema kutokana na mapingamizi hayo amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wetu wa CCM ,Rais Dk.Samia tumeona wagombea wa vyama mbalimbali wamewekea mapingamizi na yako sahihi.
"Na kwa mujibu wa Sheria makosa hayo waliokosea hawawezi kugombea.Hivyo tumekubaliana na Mwenyekiti Wizara husika inayosimamia uchaguzi kusamehe makosa madogo madogo yaliyopo katika fomu ambazo zimewekewa mapingamizi.Tunajua Wizara inasimamia sheria lakini kwa maslahi mapana ya Taifa letu ni vema wakasamehe ili wagombea wengi washiriki.
"Tunajua makosa katika uchaguzi wa mwaka huu yako mengi lakini katika uchaguzi ujao yatapungua kwani tunaendelea kujifunza na demokrasia ya nchi yetu bado changa hivyo tunayo nafasi ya kuendelea kupeana nafasi.Waziri mwenye dhamana tunatambua sheria zimefuatwa,lakini demokrasia yetu ni changa na inaendelea kukua, uchaguzi huu makosa yatakuwa mengi lakini yataendelea kupungua."amesisitiza.
Dk.Nchimbi amesema msimamo wa Chama Cha Mapinduzi ni huo na una baraka za Rais DK.Samia Suluhu Hassan huku akifafanua kuwa yeye kama Katibu Mkuu wa Chama hicho amezungumza na Mwenyekiti wa CCM Dk.Samia."Ni vema nikaeleweka vizuri nimezungumza na Mwenyekiti wetu wa Chama na ndio maana CCM tunatoa msimamo huuu."
Akijibu hoja ya wagombea wa CCM kpendelewa katika mchakato huo,Dk.Nchimbi amesema hakuna upendeleo wa aina yoyote na kwamba CCM imesimamisha wagombea katika nafasi zote zinazoshindaniwa wakati vyama vya upinzani vimeshindwa kusimamisha wagombea katika maeneo mengi.
No comments:
Post a Comment