JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAKONGO WAGOMA KUZIKA BINTI YAO

Share This
Mchungaji Kalanba Mukala Louis  ambaye ni baba wa marehemu  binti Berlis.
Baba mdogo wa marehemu  Mchungaji  Enock  Ambroseo.


Aliyekuwa Mwenyekiti  wa Jumuiya ya Wakongomani wanaoishi nchini Abdallah Serge.


Na Mwandishi Wetu
RAIA wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC) wanaoishi nchini wameweka msimamo wao wa kugoma kuzika mwili wa binti Ngalula Berliss (17) ambaye mwili wake uliokotwa hivi karibuni maeneo ya pori Msangani Wilayani Kibaha Mkoani Pwani akiwa amefariki kwa ilivyoelezwa amechomwa na kitu chenye ncha kali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 26,2024 nyumbani kwake eneo la Mkuza Muharakani baba wa marehemu aliyejitambulisha kuwa Mchungaji Kalanba Mukala Louis amesema Jumatatu iliyopita marehemu alimuaga mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 kuwa anakwenda saluni kusuka nywele .

' Hatukua na taarifa zozote hivyo nilimtuma mdogo wake aende kumuulizia kwa majirani kote hawakufahamu alipokwenda na hakuna, nikatoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa tukashirikiana kusambaza picha zake kwa majirani na wachungaji mbalimbali siku ya Jumatano Mwenyekiti alinipigia simu na kuniambia amepata taarifa kuna mwili umeokotwa mapori ya Msangani uko Hospitali ya Rufaa Tumbi Mkoa wa Pwani tukaongozana kwenda kuuangalia nilipofika chumba cha maiti nikamtambua mtoto wangu lakini nikazuiwa nisimguse kwa sababu za kiusalama niliona mwili umerowa damu huku akiwa ametobolewa macho nimelia sana" Mchungaji Louis ambaye ni baba wa marehemu Berliss.

Wakati huohuo babamdogo wa marehemu Mchungaji Enock Ambroseo amesema kuwa marehemu Berliss na baba yake wameingia nchini kwa miezi mitatu hadi umauti ulivyo mfika hivyo ni mgeni .

"Baada ya kutoa taarifa kwenye Jumuia ya Watu wa Congo tumeaamua kuwa na msimamo mmoja kwamba hatutakwenda kuchukua kibali cha mazishi ya binti yetu hadi pale uchunguzi utakapokamilika na marehemu apate stahiki zake kwa kukatishiwa uhai"amesema Ambroseo.

Alidha aliyekua Mwenyekiti wa Umoja wa Wakongomani wanaoishi nchini Abdallah Serge amesema kwa niaba ya Umoja wao wamegoma kumzika marehemu Berliss mpaka watakapo ridhika na uchunguzi wa mauaji hayo tofauti na ilivyo sasa hawajaridhika na taarifa iliyotolewa na Polisi.

"Jana usiku nimempigia simu Balozi wetu wa Congo amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha binti yetu na amesema ataandika barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje kutoa malalamiko yao" amesema Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wakongomani wanaoishi nchini.

Akizungumza kwa njia ya simu Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Pwani Muhudhwari Msuya amesema uchunguzi wa kuwabaini wahusika bado unaendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad